Posts

Showing posts from June, 2024

SAFARI YANGU YA WOKOVU

Image
  YESU ASIFIWE SANA... Nimekuwa nikikutana na jumbe za watu wakitaka niwaeleze niliokokaje? Nikashindwa kumjibu mmoja mmoja badala yake nikawa nikiwaambia nitawajibu siku. Leo ninalitimiza hilo. Kwa majina naitwa Annah steven Tewele, mwenyeji wa mkoa wa Iringa lakini kwa sasa naishi Dodoma kimasomo. Mama yangu Veronica Sanga  aliokoka  kitambo sana hata kabla hajaolewa. Enzi za ubinti wake alikuwa mtumishi wa Mungu mzuri hasa kwenye eneo la maombi. Mpaka akatuzaa watoto 4, mimi nikiwa second born, tangu udogo tulikukulia kwenye wokovu wa kurithi kwa mzazi (mama). Tusipoenda kanisani viboko, Hivyo tulikuwa tunakwenda vipindi vya watoto kila jumamosi na jumapili. Nikiwa darasa la tatu nilipata rafiki mle darasani ambaye alikuwa na kundi kama la watoto 5 hivi. Kila siku wanachanga hela (zamani hizo hela za kula shule ni 50 au 100), wakichanga watanunua miwa, vibama, mifudu na visheti kisha tunagawana. Mimi nilikuwa sipewi hela mara chache, hivyo nikienda shuleni bila hela we...

NILIVYOTOKA KUWA MUIMBA KWAYA HADI KUJIUZA NA KUKUTANA NA YESU TENA

Image
  Imesimuliwa na : AGNESS Mwandishi: CRARENCY SANGA Simu: 0742449173 YESU ASIFIWE... Mapenzi ni siraha ambayo ikiamua kutumika inaweza kuangamiza ulimwengu mzima bila hata chemb,e ya huruma. Nisikilize mimi Agness nikupitishe kwenye simulizi yangu iliyojaa milima na mabonde, pepo na asali , chungu na tamu, shubiri na asali. Naamini kuna kitu utajifunza. KIPANDE CHA KWANZA. “Kwa nini umeamua kufanya kazi hii ambayo jamii imeitenga na kuiweka kama kazi haramu”nilimuuliza baada ya kuona ukimya unazidi kutawala mule ndani “Kwa sababu wateja mpo”alinijibu huku akitabasamu “Lakini wewe ni binti mzuri mwenyewe uwezo wa kuwa na kila mwanaume unayemtaka imewezekanaje umeamua kazi hii ya kuuza utu wako”niliweka mtego wangu hapo Akaniangalia kisha akasogeza lips zake hukumkono mwingine akiwa amenishika kifua changu kisha akanipa busu papi za mdomo wangu kwa sekunde kadhaa huku akiniangalia kwa jicho la kulegea kama amekunywa kilevi kilichoanza kumzidia akasema.. “Mkaka mpole, handsome,pesa un...

USHUHUDA WA MAMA MCHUNGAJI

Image
  Bwana Yesu Asifiwe Sana... Pastor Anni Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 26, nimemaliza chuo kikuu nina degree yangu. Kwasasa nimejiajiri mwenyewe Nina ofisi yangu ya uwakala wa mitandao ya simu na Bank ambayo ni kubwa tu, so nina maisha yangu na ninaweza kujisimamia. Nilikutana na huyu kijana mwaka 2021 alikuwa anakuja sana kwenye ofisi yangu ya uwakala maeneo ya mwenge na alikuwa mteja wangu mkubwa tu, tukazoeana tukawa marafiki anakuja ofisini kwangu tunapiga story sana, mara zingine huninunulia lunch pela nakula aondoka. Tukawa karibu sana. Mara zote amekuwa akiniambia kuwa yeye ameokoka na ni Mchungaji ana kanisa analichunga na amekuwa akinisisitiza sana kuhudhuria ibada kanisani kwakwe. Pastor Anni Mimi nasali ila sio kihivyo nimekuwa naenda tu kwa Mwamposa kupokea upako sio mtu wa maombi kivilee, na huyu jamaa anaonekana nimtu wa maombi sana ni Mtumishi. Sio siri Mimi ni mzuri nimejaliwa nina shape nzuri, sura yangu inamvuto yani niko vizuri na ninajua kuvaa yani Mtumi...

YESU ALIVYONITOA KWENYE DHAMBI YA ADDICTION

Image
  Yesu Asifiwe.. Naitwa ERIC MATATIZO (Jina Lisilo Rasmi), ****** Nimezaliwa Katika Familia ya Watu Waliookoka na Mimi pia Niliokoka Mapema sana Nikiwa Mdogo, Mwaka 2014,Nikiwa Darasa la Sita Nilikutana na Marafiki Ambao Walikua wamenizidi Umri Japo Tulikua Tunasoma Darasa Moja wao Walirudia Madarasa Kadhaa, Marafiki Hao,Walinifundisha Tabia Mbaya za Kuangalia Picha za Uchi yaani PONOGRAFIA. Niliendelea na Tabia Hiyo Huku nasali na Natumika Kanisani, Mwaka 2016,Nilifanikiwa Kufaulu Shule ya Vipaji Maalumu, na Kampani yangu ya Marafiki Yote Hawakufanikiwa Kufaulu Shule Hiyo,wao Walifaulia Shule ya Kata. Huku Kidogo Nilikosa Msukumo wa Kutazama Picha za Utupu Kwasababu Watu Niliokua Natazama nao Hawakuepo Karibu Nami, Shuleni Sekondari nilipata Nafasi Kadhaa za Uongozi,Kitendo Kilichonisaidia pia Kujificha Tabia yangu ya in Kutazama Video za Utupu, Jambo la Kushangaza Kila Ilipofika Likizo Nilijihisi nipo Huru Kuendelea Kuangalia Video za Utupu na Nikaendeleza Tena Tabia Hiyo zaidi N...