YESU ALIVYONITOA KWENYE DHAMBI YA ADDICTION
Yesu Asifiwe..
Naitwa ERIC MATATIZO (Jina Lisilo Rasmi),
******
Nimezaliwa Katika Familia ya Watu Waliookoka na Mimi pia Niliokoka Mapema sana Nikiwa Mdogo,
Mwaka 2014,Nikiwa Darasa la Sita Nilikutana na Marafiki Ambao Walikua wamenizidi Umri Japo Tulikua Tunasoma Darasa Moja wao Walirudia Madarasa Kadhaa,
Marafiki Hao,Walinifundisha Tabia Mbaya za Kuangalia Picha za Uchi yaani PONOGRAFIA.
Niliendelea na Tabia Hiyo Huku nasali na Natumika Kanisani,
Mwaka 2016,Nilifanikiwa Kufaulu Shule ya Vipaji Maalumu, na Kampani yangu ya Marafiki Yote Hawakufanikiwa Kufaulu Shule Hiyo,wao Walifaulia Shule ya Kata.
Huku Kidogo Nilikosa Msukumo wa Kutazama Picha za Utupu Kwasababu Watu Niliokua Natazama nao Hawakuepo Karibu Nami,
Shuleni Sekondari nilipata Nafasi Kadhaa za Uongozi,Kitendo Kilichonisaidia pia Kujificha Tabia yangu ya in Kutazama Video za Utupu,
Jambo la Kushangaza Kila Ilipofika Likizo Nilijihisi nipo Huru Kuendelea Kuangalia Video za Utupu na Nikaendeleza Tena Tabia Hiyo zaidi Nikaanza na KUJICHUA Kwani Hakukua na Mtumishi wa Kuniona kwa Ukaribu.
Ilipofika Mwaka 2018,Kipindi cha Easter Conference,Niliamua na Kumaanisha Kutokea Moyoni Kumtafuta Yesu abadilishe Maisha Yangu.
Hapo Ndipo Nilipokutana na Neema ya Mungu,Na Kunisaidia Kuweza Kuacha Kabisa Tabia ya Kuangalia Video za Utupu.
Ninachoweza Kuwashauri Vijana Wenzangu,ni Kwamba Kuna Aina ya Uraibu Hauwezi Kutoka Kwako Kama Usipokutana na Neema ya Kristo Yesu Moja Kwa Moja.
Neema ya Mungu inatufundisha Kukataaa Ubaya wa Kila Aina Ikiwemo na Tabia za Kiuraibu Kama Kuangalia Video za Ngono(Tito 2:11-12)
Mwanadamu Pekee yake Hauwezi Kujitahidi Kutoka Katika Tabia Mbaya kwa Nguvu Zako, ni Mpaka Neema ya Mungu iwe Juu Yako.
Kwahiyo Jambo la Kwanza ni Azimia Moyoni Mwako Kuacha Tabia Mbaya,Kisha Jambo la Pili iombe Neema ya Mungu Ije Kwenye Maisha yako,Tatu omba Neema ya Mungu Iue Hali ya Dhambi na iweke Uhai Ndani Yako Kwa Habari ya Kristo.
Ameen Ubarikiwe.

Comments
Post a Comment