Posts

Showing posts from June, 2022

JINSI NILIVYOTAHADHARISHWA KABLA YA AJALI

Image
"Rafiki yangu ambae ni mtumishi wa Mungu, alinionya sana juu ya kudharau ndoto. Alinisihi tuchukue hatua ya kuomba. Basi, tulichukua wakati tukafunga maombi.." YESU APEWE SIFA., Mimi ninafanya kazi ya UWAKALA wa mitandao ya simu yaani M-PESA, TIGOPESA, Airtel Money na HALOPESA. Siku moja nikiwa nimelala nikaota ndoto moja ambayo haikunifadhaisha sana na nikaichukulia kirahisi bila tija yoyote.  “Tazama, nilikuwa katika kibanda changu nikiendelea na kazi yangu ya uwakala kama kawaida. Kibanda changu kilikuwa mtaani kando ya barabara. Nikiwa ndani ya kibanda, ilitokea gari likiwa kwenye mwendokasi wa ajabu kana kwamba limekatwa breki. Lilianguka na kuanza kubiringika kuja uelekeo wa kibanda changu hali nimo ndani yake. Kabla gari lile halijanifikia, nilishtuka kutoka usingizini.”  Niliwaza lakini nikachukulia ni ndoto tu, na asubuhi nikaenda kuendelea na kazi kama kawaida. Siku moja wakati napiga storin a Rafiki yangu ambae ni mtumishi wa Mungu, alinionya s...

RAFIKI YANGU ASIYEONEKANA KWA MACHO

Image
  “Ndoto! ndoto! siku fulani nilipanga kuamka saa tisa alfajiri kuwa na mda na rafiki yangu asiyeonekana. ilipofika saa tisa juu ya alama nilishtuka. uchovu niliokuwa nao ulinifanya niendelee kulala. ndani ya dakika 37 za kulala huko niliota ndoto ifuatayo….”   YESU ASIFIWE., llikuwa ni usiku mmoja mtulivu majira ya tisa alfajiri nikiwa narejea nyumbani gafla niliona majitu mawili yenye nguvu yamevalia mavazi ya jeshi. bila kujua kosa nililotenda amri ilitolewa nikalala chini kifudifudi na kuchapwa viboko viwili. nikiwa pale chini nimelala pasi kujua hatima yangu niliyaona yale majitu kama yakijadili kufanya ubaya flani. yakiwa yamezubaa nilipata fursa ya kuyaponyoka na kutimua kuvumbi kuendeleza safari yangu kuelekea nyumbani. nikiwa njiani nilipita njia iliyokuwa na maziko na kumkuta mrimbwende mmoja amefichama kando ya mti.  alivyoniona alianza nishutumu mimi kuwa sababu ya mambo yake yanayokwenda mkama. nilivyomtaka athibitishe amejuaje kuwa mimi ndiye c...

JINSI JENGO LA BWENI LILIVYOPOROMOKA NIKIWA NDANI YA DARI.

Image
"Nilikaa katika dari nikichaji simu yangu. Nilisikia miungurumo kwa mbali, nikidhania huenda bi gari linapita barabarani huko nje. Lakin baada ya sekunde kadhaa, haikuwa miungurumo ya kawaida. Punde si punde, miungurumo ilizidi kuwa mikubwa.." Bwana Yesu asifiwe sana.,  Naitwa FELIX NTIRUBAZA (Kigoma, Tanzania) ilikuwa ni septemba 2016. Siku moja siku ya jumamosi mchana, mimi na wanafunzi wenzangu wachache, tulikuwa na kipindi cha vitendo maabara (Ilikuwa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, Bukoba mjini). Baada ya kujifunza mida ya saa kumi alasiri, nilishuka mpaka bwenini ili nikapumzike. Bwenini pale, kulikuwa na wenzangu wachache walokuwa wakifanya maongezi tu ya kawaida. Nilifika kitandani kwangu (nilikuwa nalala kitanda cha chini) na kulala. Baada ya kujilaza tu, wazo liliniingia kusema kwamba niende mjini. Lakin nililipinga wazo hilo kwakuwa sikuwa na ratiba yoyote ya kwenda mjini wala sikuwa na jambo lolote la kwenda kufanya mjini. Nadhiri il...

MADAKTARI WALIJIFUNZA KUTOKANA NA HALI YANGU YA KUKARIBIA KIFO

Image
“Siku iliyofuata kiwango changu cha hemoglobini kilikuwa kimeshuka hadi 2.9. Nilipoamka na kupata familia yangu yote kando ya kitanda changu, nilijiuliza ni nini kilikuwa kimetokea. Singeweza kuzungumza kwa sababu ya mashine ya kusaidia kupumua. Nilihisi hisia nyingi mno kwa huzuni, lakini singeweza hata kulia. Kila mtu aliniambia kwamba ilikuwa lazima nihifadhi nguvu zangu ili niweze kuokoka..”  BWANA YESU ASIFIWE SANA., Tulipata kujua kwamba tulikuwa tukitazamia mtoto wetu wa nne. Mtoto wetu mdogo Zaidi Mikael, alikuwa na umri wa miaka tisa, na mabinti wetu pacha, Maria na Sara, walikuwa na miaka 13. Ingawa mtoto mwingine hakuwa amepangiwa, baada ya muda mfupi tulikuja kuzoea wazo la kuwa na mtoto mwingine. Jioni moja katika mwezi wa tatu wa mimba, nilihisi maumivu ya ghafula katika pafu langu. Siku iliyofuata singeweza kutembea hata kidogo.  Daktari alisema kwamba nilikuwa na mchochota wa pafu, kisha akanipa Peninsilini. Nilianza kuhisi vema baada ya siku kadh...

MAISHA YANAVYONITESA KWA SASA.

Image
  “Ni kawaida kwa watu kutafuta hamasa kutoka kwa waliofanikiwa peke yao kwa sababu tunaamini ndio wanaijua njia sahihi ya mafanikio. Binafsi sijafanikiwa kiwango cha kutoa hamasa hiyo kwa wengine lakini nina Imani kuna mtu aliyekata tamaa kabisa atapata nguvu ya kupambana kwa kujua kuwa hayupo peke yake kwenye haya mapambano Mungu ataleta neema yake siku za mbele asilale, karibu jitahidi kusoma ushuhuda wote...”  Yesu asifiwe sana., Binafsi niliamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa baada ya kumaliza chuo kwamba nitapata kazi na kila mazuri niliyotamani yatakuja hasa kuiheshimisha familia yangu lakini hali imekua tofauti kila kukicha afadhali ya jana, nimetembeza sana vyeti hadi kuomba kazi ikageuka kazi yenyewe ubaya haina mshahara. Kila mpango niliojaribu kufanya iwe biashara au wazo lolote hakuna linapofanikiwa mpaka rafiki zangu wakaanza kuniita Utopianist (wakimaanisha mtu mwenye mawazo ya ujamaa ambayo hayatekelezeki). Kila ninachogusa hakiendi ilifika ...

NINAWEZAJE KUPATA FARAJA NA AMANI, WAKATI MWENZANGU AMEKUTWA NA KIFO?

Image
Yesu asifiwe sana.., Hata kama tunahakikishiwa kuwa mpendwa wetu yuko mahali pazuri, bado tunapata maumivu ya kutokuwapo kwake duniani. Ni sawa kuomboleza upotevu wa mpendwa wako. Yesu alilia juu ya kifo cha Lazaro, hata akijua kwamba atamfufua Lazaro. Mungu haogopi hisia zetu au maswali yetu. Tunaweza kumtunika mizigo yetu na kuamini katika upendo Wake ili kutupatia uhakikisho na faraja (1 Petro 5: 7). Tunaweza kukumbuka mambo mema mengi kuhusu wapendwa wetu waliopotea na kufurahi katika ukweli kwamba tuliweza kushiriki katika maisha yao.  Tunaweza kushiriki hadithi za ushawishi wa wapendwa wetu juu maisha yetu. Tunaweza kupata faraja ya kufanya baadhi ya vitu ambavyo wapendwa wetu waliopotea walifurahia hasa au kutumia wakati wa ukumbusho kuhusu wapendwa wetu waliopotea na jamaa na marafiki wengine wa karibu. Tunaweza pia kuheshimu kumbukumbu zao kwa kuishi maisha yetu kwa njia inayoleta heshima na utukufu kwa Mungu. Ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu hatimaye ndiye c...

TATIZO LINALOWAKUMBA VIJANA WENGI BAADA YA KUOKOKA

Image
 Kuna tatizo sugu ambalo linalowasumbua watu wengi , hususani vijana pindi wanapookoka, Na pengine linakusumbua hata na wewe. Vijana kadha wa kadha waliookoka, wamekuwa wakinipigia simu, wengine wakinitumia meseji wakisema mtumishi, tangu nilipookoka, nimejitahidi kweli kuacha uasherati na kutazama picha chafu (za ngono) mitandaoni, Lakini naona kama ninamkosea Mungu kwasababu, zile taswira za yale niliyokuwa ninayafanya au ninayatazama, zinanijia mara kwa mara akilini mwangu, wakati mwingine hata wakati nikiwa naomba, au najifunza Neno.   Hivyo naona kama bado sijakamilika, Mungu hajanisamehe na kuniosha dhambi zangu, najisikia vibaya sana, imenipelekea kukosa nguvu ya kumtumikia Mungu.. Nifanye nini? Kama na wewe umekuwa na tatizo kama hili nataka nikuambie, wewe sio wa kwanza, Biblia inasema mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru.(Yohana 8:32) Jambo ambalo wengi hatufahamu ni kuwa, Utakaso wa Mungu umegawanyika katika sehemu mbili. Upo utaka...