Posts

Showing posts from June, 2026

WALINICHOMA KISU MARA NNE

Image
  Naitwa Moza, ni msukuma wa Bariadi. Sawa , mwaka 2022 nilimaliza chuo DUCE nakumbuka wiki moja kabla sijamaliza mtihani wangu wa mwisho wa UE, nilipigiwa simu na shangazi yangu aishiye Iringa mjini kwamba nimalizapo mitihani niende iringa nikamtembelee. Nikaona ni vyema sana maana mara ya mwisho yeye kuja Bariadi ilikuwa kipindi niko sekondari. Iliniongezea ulazima wa kwenda maana shangazi pia alikuwa amefiwa na watoto wake watatu tena vifo vya kutatanisha. Hivyo mimi kwenda ilikuwa namna pia ya kumtia moyo. Miaka yote nilipokuwa nakua, kwenye familia yetu kulikuwa na migogoro kati ya ndugu upande wa baba na upande wa mama . Nilikuwa sielewi nini haswa kilitokea huko nyuma . Nilijaribu kumuuliza mama shida ni nini lakini mama alinisihi kupuuza tu maisha yaendelee.  wiki moja baadae nilikuwa nimeshamaliza mambo yote ya chuo. Nilipanda bus mpaka Iringa. Baada ya kufika Iringa shangazi alikuwa ameshanijulisha kuwa atamwagiza dereva ambaye ni rafiki yake anifuate anipeleke hadi ...

NILIWAZA KUJIUA NILIPOKUWA NA MIAKA 13 TU

Image
  Jina langu ni Sanjo Mlimba, mwenyeji  wa Kisesa, Mwanza. Hadithi yangu ilianza zamani sana kabla sijaathirika na uraibu wa madawa . Nakumbuka Nilikuwa na umri wa miaka 13 tu nilipowaza kwa mara ya kwanza kujiua. Sikuelewa ule upweke niliokuwa nao kipindi hicho ulitokana na nini .Nilikuwa sipendi kabisa kuchangamana na watu kabisa. sikuwa na marafiki , hata nikiwa nyumbani nilikuwa napenda kukaa mwenyewe chumbani. Nikiwa shule, kuna wakati naweza kutoka tu darasani nikaenda kukaa kichakani mwenyewe.  lakini sasa naona kwamba adui alikuwa  anajaribu kuikatisha stori yangu kabla hata haijaanza vizuri. Kuna wakati nilikuwa naona kuishi duniani hakuna maana yoyote. Naona tunaenda shule kila siku, mara watu wanaenda mjini wanarudi ,watu wanaenda ziwani kuvua mara shamba hayo yote kwangu nilikuwa naona hayana maana kabisa .Sijui nilikuwa na pepo gani ila ni kwamba nilikuwa sion maana yoyote ya kuishi. Siku moja nikiwa darasa la sita , niliamka mapema kwenda shule kama kaw...