USHUHUDA WA MAMA MCHUNGAJI

 


Bwana Yesu Asifiwe Sana...

Pastor Anni Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 26, nimemaliza chuo kikuu nina degree yangu. Kwasasa nimejiajiri mwenyewe Nina ofisi yangu ya uwakala wa mitandao ya simu na Bank ambayo ni kubwa tu, so nina maisha yangu na ninaweza kujisimamia. Nilikutana na huyu kijana mwaka 2021 alikuwa anakuja sana kwenye ofisi yangu ya uwakala maeneo ya mwenge na alikuwa mteja wangu mkubwa tu, tukazoeana tukawa marafiki anakuja ofisini kwangu tunapiga story sana, mara zingine huninunulia lunch pela nakula aondoka. Tukawa karibu sana.

Mara zote amekuwa akiniambia kuwa yeye ameokoka na ni Mchungaji ana kanisa analichunga na amekuwa akinisisitiza sana kuhudhuria ibada kanisani kwakwe.

Pastor Anni Mimi nasali ila sio kihivyo nimekuwa naenda tu kwa Mwamposa kupokea upako sio mtu wa maombi kivilee, na huyu jamaa anaonekana nimtu wa maombi sana ni Mtumishi. Sio siri Mimi ni mzuri nimejaliwa nina shape nzuri, sura yangu inamvuto yani niko vizuri na ninajua kuvaa yani Mtumishi alikuwa akija ofisini kwangu unamuona kabisa anavyo changanyikiwa.

Baada ya kuzoeana kwa muda aliniambia ananipenda na anataka kunioa, na akasema kanipendea uchapakazi wangu na usmart wangu, na Mimi kwakweli nilimpenda ni mwanaume handsome na smart. Basi mahusiano yetu yakaanzia hapo.

Baada ya muda Mtumishi akaanza wivu anakuja ofisini kwangu bila taarifa na akiniona naongea na wanaume anaumia mpaka anatoa machozi, kwakweli nilikuwa namuonea huruma maana alionyesha kunipenda sana. Akinipigia simu nisipopokea nitakuwa na kazi kubwa ya kumbembeleza. Siku zikaenda akaforce aje kwetu akatoa Mahari process za ndoa zikaanza. Nikamshukuru Mungu kunipatia Mume mwema tena Mtumishi. Kwakweli tulienjoy sana uchumba wetu yani nikasema kuolewa na Mtumishi ni raha sana nilijihisi niko paradiso.

Sasa kasheshe ikaanza ikabidi anipeleke kanisani kwake anitambulishe kwa viongozi wa kanisa na washirika. So wakati tunakaribia kufunga ndoa ikabidi niwe nasali kanisani kwake ili nipazoee. Siku ya kwanza naingia lile kanisa nikaona baadhi ya wadada wamekasirika vibaya, wengine hata vigelegele hawapigi, na wengine hata nikiwasalimia hawaitikii, sikuona kama nishida nikaamua kunyamaza niendelee na maandalizi ya harusi yangu. Nikatulia mpaka harusi ikafanyika tukaenda honeymoon na baadae tukarudi kanisani.

Balaa lilianzia hapo, kuna wamama wawili hapa kanisani mmoja ni Mzee wa kanisa na mwingine ni Mwenyekiti wa wamama, wanawake hawa wanauwezo kifedha na wamekuwa wanamsupport sana Mchungaji. Yani wamekuwa wakitoa fedha zao, wanaenda kufanya usafi kwenye nyumba ya Mtumishi, wanapika na mambo mengi kama hayo, na mume wangu hakuwahi kunieleza hili swala.

Sasa nimeolewa niko nyumbani kwangu siku ya kwanza wakaja wale wamama wakaanza kupiga deki, kuosha vyombo wakachukua nguo za Mchungaji wakafua, wakapika na chakula wakala na Mchungaji, kiukweli nilishangaa lakini pia nilimshangaa Mume wangu anaruhusi vipi watu kuwa huru na nyumba yetu kiasi hiki. Ila nikajua kwasababu ni maharusi wapya watatuacha.

Hawa wamama wameendelea na hiyo desturi ya kuja kwangu au kutuma mabinti wakanisani kuja kumuhudumia Mchungaji. Mpaka jumapili wanaleta chai, chakula cha mchana mpaka jioni. Wanamnunulia Mume wangu nguo, viatu na kila kitu hadi vocha za simu wanamuwekea. Mimi binafsi sikufurahishwa kwani nilakaa miezi mitatu sijafua nguo za mume wangu, sijampikia, nikisema nipike chakula kile chakula nitakula mwenyewe maana wale wamama wanaleta makuku ya kienyeji, nyama ya mbuzi, mayai

yani vitu kibao. Na Mume wangu alionyesha kuwahusudu na kuwaogopa kwa namna Fulani. Hichi kitendo kiliniuma sana!!!!!! Nikifanya kitu wanaanza kunikosoa Mchungaji hali chakula hicho, sijui chai yake iwe hivi yani nyumba yangu lakini walimu wengi

Tulifunga ndoa na Mume wangu mwaka jana 2022 mwezi wa tatu hivyo mpaka sasa ndoa yetu ina mwaka mmoja ni miezi kama saba hivi.

Waliendelea na tabia yao ya kuja kwangu, so ikafikia hatua Mimi nikiamka asubuhi najiandaa naenda zangu kwenye biashara zangu maana wakumuhudumia mume wapo, na saa zingine wakija pale hata hawanisalimii wanaingia moja kwa moja jikoni kuendelea na kazi.

Kuna siku nilikaa na mume wangu nikamwambia sipendi hawa watu wanavyokuja hapa nyumbani kwangu nakuwa siko huru na nyumba yangu, akaniambia waache ni watoto wangu wakiroho hawakuhusu waache. So nikanyamaza na nikamuona Mchungaji kakasirika kabisa Mimi kumwambia hivyo.

Kanisani wale wamama hawanishirikishi chochote Mwenyekiti wa wamama anapanga program za wamama wanafanya vitu Mimi sijui chochote, yani pale kanisani nilitengwa mpaka najiona kama natengwa.

Kuna siku usiku tumelala kama saa nane hivi yuke Mama Mzee wa kanisa akampigia simu Mume wangu akasema anajambo Mungu kamuonyesha

wakati anaomba hivyo anataka kuja asubuhi kumueleza, Mchungaji akasema sawa. Basi asubuhi ilipofika yuke Mama alikuja ila alibeba kuku wa kienyeji akaingia jikoni akapika supu akatenga akanywa na Mchungaji yotee wakamaliza hawakubakisha hata kidogo, wakaongea wakamaliza akaondoka. Baada ya yale maongezi nikaona Mchungaji kabadilika kabisa hanisemeshi tena akiingia ndani amenuna, nikimpigia simu ananijibu kwa ukali kwakweli sikuelewa kuna nini. Na baada ya muda wakaja kikundi cha wamama wanamaombi na mzee wakanisani na yule Mwenyekiti, siku hiyo walifanya usafi nyumba nzima, wekapika, wakafua halafu wakaanza maombi wanavunja nguvu zote za kichawi na kila roho inayoharibu kanisa. Imagine asubuhi unaamka unakuta watu wanapiga kelele wanaomba nyumbani kwako. Mimi nikaamka nikajiandaa huyu nikaenda kazini.

Sio siri nilianza kuchoka na kuchukia hii ndoa. Kuna siku Mume wangu aliumwa alipata mafua makali na homa alikuwa anatetemeka akawa hawezi hata shika simu, ilikuwa usiku ikabidi nimuogeshe nimpe dawa alalee, ilikuwa siku ya kwanza tangu kuolewa kumuhudumia mume wangu, nilimpikia uji akanywa. Sasa wakati kalala nikachukua simu nikaanza soma msg, nikakuta Mama Mzee wa kanisa anamwambia Mume wangu Mimi nina tumikishwa kichawi, nina madhabahu za kwetu zitaharibu kanisa, na wakamwambia ahakikishe hali kitu chochote kutoka kwangu maana vyakula vyangu vina uchawi utaua huduma yake. Nikasoma msg nyingine Mama

mwingine kamtumia Mchungaji Mungu kanionyesha mkeo ni Maria wa praise huyu ulieoa sio yani ataua huduma. Nilijisikia hasira sana. Nikajua kumbe hawa watu wamefika mbali. Sio siri roho iliniuma sana hasa baada ya kujua sio watu wazuri kwangu.

Nikaanza kuwa jeuri, siku hiyo nikasema siendi kazini leo nabaki na huyu Baba, asubuhi nikaamka nikafunga geti nikafunga milango na simu ya Mchungaji nikaishika Mimi, nikamwamsha nikamuogeaha nikampikia chai akanywa, wale wamekaa getini wanagonga sifungui, Mchungaji akalala namimi nikalala nikasema leo ndio watanijua. Baadae Mchungaji akaamka akasema hawajaja hawa watu nikasema hawajaja kumbe wako nje ilikuwa jumamosi Kesho yake jumapili, nikapika mchana tukala tukapumzika, ikafika saa tisa nikatoka nikafungua geti nikakuta wamejaa nje wanataka kuingia, nilipofungua wakanisukuma kwa hasira wakaenda mpaka chumbani wakaanza kumuuliza Mchungaji anaendeleaje mara wakamchukua wakaenda nae hospital, Mimi wameniacha ndani wengine wakaanza kupika chakula kingine waliporudi wakanikuta nimetulia. Wakaanza kuomba mmoja akasema Mchungaji kalishwa kitu kibaya kitapelekea nguvu zake kupungua, mwingine Mchungaji kwafungwa na uchawi basi wakaanza kukemea pale weeeeh nawaangalia tu.

Sio siri hasira zikanipanda, mpaka ikapelekea Mimi kufanya hivi.

KISA CHA MAMA MCHUNGAJI - MWISHO

Sio siri Pastor Anni ule usiku sikulala nilikuwa nalia tu, naumia maana Mimi sina mapepo, sijui uchawi na familia yangu haiamini uchawi inakuwaje watu wanakaa sebleni kwangu wanaanza kuomba na kunikemea Mimi mchawi. Nilikasirika sana.

Sasa kuna Dada yangu mmoja anaitwa Janet yeye yuko tabata tuko karibu sana, nilishawahi mueleza matatizo yangu akaniambia nyenyekea tu baadae wataacha. Sasa huo usiku nikampigia nikamueleza kilichotokea akasema kwakweli hapo hapana wanaelekea pabaya onyesha makucha yako wasikuzoee. Nikasema sasa watanijua,

Ikafika jumapili nikajiandaa kwenda kanisani Mume wangu alikuwa bado anamafua na alikuwa weak, nikaandaa chai hakunywa basi nikaamua nimkamulie juice ya machungwa na chupa nyingine nikambebea maji nikasema atakunywa kanisani.

Sasa ibada ikiwa inaendelea tumekaa mbele na mume wangu nikaamua nitoe ile chupa ya maji na juice niweke mezani ili anywe kabla hajasimama kuhubiri, weeeh akatokea Mama Mzee wakanisa mbio na chupa ya maji ya afya na glass akazitoa zile chupa zangu, nikasimama nikamuuliza unapeleka

wapi chupa zangu, akasema Mchungaji ana maji yake haya hapa nikamwambia atakunywa haya niliyomuwekea Mimi mke wake, nikamuona anielewi anataka kuondoka na chupa zangu nikasimama nikamzabua yule Mama kibao kimoja usoni paaah nikamwabia acha chupa hizi, hakuelewa nikampa kibao kingine paaah nikasema acha chupa hiyo na toa uchafu wako. Yule Mama akaanza kulia akaja Mwenyekiti wa wamama nikampa kibao cha uso paaaah nikamkunja shingoni nikamwambia nitakuumiza toeni uchafu wenu.

Basi watu wakatuamulia, nikatoka nikamfwata yule Bint Maria wa Praise wanaesema anafaa kuwa mke wa Mchungaji nikampa vibao viwili vya maana nikawa namtafuta Mwenyekiti wa maombi, kifupi niliuwasha moto basi wakanishika wakanitoa nje, Mchungaji akasema nina tatizo la akili basi wakaanza maombi wacha wanikemeee kifupi ibada ili iharibika wakaanza kuniombea na kunikemea Mimi pepo.

Nikaone isiwe shija nikarudi nyumbani nikapumzika maana nilikuwa na hasira. Usiku ukafika mmewangu hajarudi nyumbani, jumatatu, jumanne kimya na simu hapokei. Kuna kijana mmoja kanisani yupo muda mrefu yeye tuko vizuri na ananielewa nikamtumia elfu 20 nikamwambia fwatilia Mchungaji alipo nijulishe. Baadae akanipigia akasema yuko Goba yuko kwenye nyumba ya Mzee wa kanisa wanawafanya maombi viongozi wote wa kanisa nikasema sawa. Akanipa location nikajiandaa huyoo mpaka Goba.

Nikafika ni nyumba mpya kama apartment nikagonga geti mlinzi akafungua nikaingia ndani nikagonga mlango wa sebleni akaja mtu kufungua huyo aliye fungua alivyoniona katoka mbio kakimbia ndani, nikaingia sebleni nikawakuta wengine wawili wakatoka mbio nje yani kama wameona gaidi 😂😂😂. Ila chakushangaza hakukuwa na maombi wala nini, nikaanza fungua chumba kimoja kimoja sioni mtu, nikagonga chumba kimoja maana kilikuwa kimefungwa akafungua Mchungaji alivyoniona akataka kuufunga nikausukuma nikaingia ndani, Mume wangu akajitupa kitandani akasema umefwata nini hapa umekuja kuniua niue sasa, weeeh nililia nikamwambia mume wangu mimi nakutaka wewe, nakupenda Mume wangu. Akasema hapana hunipendi na unataka kuharibu huduma yangu. Akaniambia Mimi nimehama nyumba kanisa limenipangia nyumba nyingine, ile nyumba kaa kodi ikiisha hama tafuta pakukaa. Na kanisani nisikuone tena yani upotee. Niliishiwa nguvu, nililia sana nikamuomba mume wangu msamaha, nililia na kugalagala akasema lia ukimaliza ondoka wewe sio mke.

Basi niliondoka kurudi nyumbani Mume wangu hakuja, baada ya wiki mbili akaja kubeba vitu vyake na nikaambiwa nihame kwenye nyumba mwenyewe anaitaka so nikabeba vitu vyangu nikapeleka nyumbani kwetu, mume simuoni, hanitaki naonekana shetani, kanisani siruhusiwi kwenda. Nipo tu. Ndoa ya Mchungaji ndani ya mwaka mmoja imeisha kama hivyo.

Kwasasa niko naishi mwenyewe Mume hatuna mawasiliano na sijui hatma ya ndoa yangu nimeamua nitulie tu kwanza upepo upite.

MWISHO

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

JE, UNA USHUHUDA AMBAO UNGEPENDA TUUCHAPISHE?? 
 Fanya hivyo ili maelfu wajue mambo ambayo MUNGU alikutendea na kupitia ushuhuda wako  maelfu ya wasomaji  watayashuhudia matendo ya  Mungu uliyenaye. 
Endapo unao Ushuhuda tafadhali BOFYA HAPA


Comments

Popular posts from this blog

SAFARI YANGU YA WOKOVU

NILIVYOTOKA KUWA MUIMBA KWAYA HADI KUJIUZA NA KUKUTANA NA YESU TENA