NILIVYOTOKA KUWA MUIMBA KWAYA HADI KUJIUZA NA KUKUTANA NA YESU TENA
Imesimuliwa na : AGNESS
Mwandishi: CRARENCY SANGA
Simu: 0742449173
YESU ASIFIWE...
Mapenzi ni siraha ambayo ikiamua kutumika inaweza kuangamiza ulimwengu mzima bila hata chemb,e ya huruma. Nisikilize mimi Agness nikupitishe kwenye simulizi yangu iliyojaa milima na mabonde, pepo na asali , chungu na tamu, shubiri na asali. Naamini kuna kitu utajifunza.
KIPANDE CHA KWANZA.
“Kwa nini umeamua kufanya kazi hii ambayo jamii imeitenga na kuiweka kama kazi haramu”nilimuuliza baada ya kuona ukimya unazidi kutawala mule ndani
“Kwa sababu wateja mpo”alinijibu huku akitabasamu
“Lakini wewe ni binti mzuri mwenyewe uwezo wa kuwa na kila mwanaume unayemtaka
imewezekanaje umeamua kazi hii ya kuuza utu wako”niliweka mtego wangu hapo
Akaniangalia kisha akasogeza lips zake hukumkono mwingine akiwa amenishika kifua changu kisha akanipa busu papi za mdomo wangu kwa sekunde kadhaa huku akiniangalia kwa jicho la kulegea kama amekunywa kilevi kilichoanza kumzidia akasema..
“Mkaka mpole, handsome,pesa unazo lakini hufananii kuwa mteja wa hizi huduma kipi kimekupelekea kuwa hivo na hakuna msichana anaweza kukukataa”Lile swali nililomuuliza sasa lilikuwa limekuja kwa upande wangu Sikushaangaa kwa nini hajanijibu kwa sababu nawajua watanzania huwa hawajibu swali kama hawajauliza swali.Ndio tunajijua wenyewe huwa tunajibu swali kwa swali
“Kwahiyo unanambia sababu zilizosababisha mimi kuwa mteja wa huku na wewe ndio zilezile zilizosababisha ufanye biashara hii”nilimuuliza huku nilitarajia kujibiwa kwa swali kama alivyofanya mwanzo
“Hapana sijajua kwa upande wako ila kwa upande wangu nimechoka kuwa mtumwa wa hisia zangu,Kama kwenye mapenzi nishakuwa na kila aina ya wanaume na nishafanya kila ambacho mwanamke anatakiwa kufanya lakini niliishia kuumizwa tu”alionge huku akiwa na dalili za kutokwa na machozi. Ilikuwa ni saa nne na nusu usiku ndio saa yangu ya ukutani ilinambia,hata mawazo yangu yalikuwa yamemakinika sana na mjongeo wa saa ile
“Vipi kuhusu wewe”Agnes aliweka swali mezani huku akionekana kama mtu mwenye kiu ya kutaka kujua nini kimenikumba.
Ilikuwa ni kama nafasi adhimu niliyokuwa naisubiri kwa miaka mingi ije itokee na mimi nipate walau mtu atakayenipa muda wa kuyasikiliza ya moyoni mwangu yaliyokuwa ya kinitesa kila siku.Ndugu msomaji katika maisha WATU wanapitia vitu vingi sana, kama kuna mtu atahitaji
kukueleza kile anachokiita tafadhali tenga muda wako umsikilize huenda utakuwaumemsaidia kuutua mzigo mkubwa sana alioubeba.
“Ni kama wewe tu mapenzi yalikuwa kama Kinga ya mwili wangu,kila niliye mwamini aliondoka na moyo wangu na kwenda kuupiga mnada kwa bei rahisi mno”niliongea kisha nikamuangalia usoni na kumrushia swali lingine
“Hii biashara umeanza lini”
“Leo”alinijibu huku akishindwa kuzuia machozi yake kutoka na kilio cha kwikwi kikianza wa mbali
Sikutaka kujua kama amenipa jibu la uwongo au la ukweli nilichotaka ni kujua ni historia yake iliyomsukuma kufanya vile
“Mimi ni mteja wako wa ngapi kwa leo” “Wa kwanza”alinijibu Sikuwa na mashaka sana na jibu lake kwani hata kwenye ila application yakununua wadada wanafanya hii biashara ilikuwa ni mara ya kwanza namuona katika orodha ya wale niliowazoea
“Kwa nini ukachagua hii biashara”nilimuuliza “Samahani umeniambia unitwa nani”
“Pocha ndio jina langu”nilimjibu huku nikitaka nijue historia yake
“Sawa Pocha ipo hivi….. ANASIMULIA AGNES.
Wakati nikiwa bado mtoto nilikuwa nikisikia watu wamejiua kisa mapenzi niliona ni watu ambao hawana utimamu vizuri wa akili,ndio nilidhani hivyo.Kila aliyetoa Machozi kisa mapenzi nilimuoana ni limbukeni asiye na matumizi sahihi ya Machozi yake zaidi zaidi niliishia kumcheka tu.
Kadri nilivyodhidi kuikaribia balehe nazo tamaa za kimwili zikanivaa bila kusubiri niishi balehe yangu vizuri. Katika umri wangu mdogo tu miaka kumi na miwili chuchu zilikuwa zimeshaanza kuwatanisha vijana wa mtaani wenye tamaa nao hawakusita kuja kubisha hodi kwangu.
Mwanzo niliweka msimamo mkubwa sana lakini nikiwa na miaka kumi na mitatu kitasa changu kikavunjwa kwa mara ya kwanza. Nakumbuka nikiwa kidato cha kwanza ndio kwa mara ya kwanza nimeingia kwenye mapenzi na Peter mkaka aliyenizidi vidato viwili mbele yangu
Nae alipomaliza haja za moyo wake baada ya kumaliza kidato cha nne akapotelea mitini, aliikimbia huku akiwa ameshautoa usichana wangu. Huyu sitamuhesabu sana katika mahusiano yangu na baada ya hapo hata wale niliochezeana nao hapo shuleni sitawahesabu maana nilijipa ujasiri ya kwamba wameujenga moyo wangu na nitaweza kuvumilia maumivu yoyote ya mapenzi kumbe nilikuwa sijayaishi maumivu ya mapenzi hata kidogo.
Nikiwa na miaka kumi na nane hapo ndipo dunia ilileta walimu kamili wa kunifundisha misamiati ya mapenzi na maana yake Kwa mara ya kwanza namtia machoni Patrick mwanaume mpole na anayemjua Mungu niliamini nimepata Mume wa maisha yangu yote ya hapa Duniani, Mume nitakaemaliza nae safari nzima ya mapitio hapa duniani.
Nilikutana nae kanisani kwenye zile ibada za jioni. Siku ya kwanza tunakutana nae aliomba awe
mwenyeji wangu maana mimi ndio ilikuwa mara ya kwanza nahudhuria ibada ile nami bila pingamizi nikakubali Kila usiku alikuwa ananipigia na kunifundisha mafundisho ya kiroho zaidi nami nikakuwa kiroho siku hadi siku. Kadri siku zinavyozidi kwenda nami nikaufungua moyo wangu kwa Patrick hata alivyokuja
kunieleza kuwa anataka awe nami kwenye mahusiano mimi nilikuwa nishamuelewa zamani sana. Ilikuwa ni kama kumsukuma mlevi tu tena kwenye mteremko mkali.
Hapo baada ya kukaa mda mrefu bila kuwa kwenye mahusiano nikajikita katika kisiwa cha mapenzi yake..
“Ichunge sana tamaa yako, itakuongoza ndani ya dakika chache kufanya jambo, lakini litakugharimu kwenye Maisha yako..”
Kila penzi jipya huwa ni tamu, Patrick alikuwa ni kama box kamili lililokuja likiwa na kila kifaa chake na kusahaulika kitu kimoja tu cha muhimu.Ni kama television iliyokuja bila remote basi ndivyo Patrick alivyokuja bila uaminifu. Muhusiano yetu yalikuwa ni ya siri baina yetu mimi na yeye tu hakutaka kuyaweka hadharani kila nilipogusia suala ya kuyaweka wazi ilikuwa ni kama kidondo kilichotiwa pilipili hakutaka kabisa suala hilo ndio ulikuwa ugomvi wetu mkubwa baina yangu na yake. Tulifanya kila wanandoa walichotakiwa kufanya bila kujari mafundisho ya kanisani yanakataza tukaweka dini kando tukayafurahia mapenzi yetu. Patrick huyu wa saivi alikuwa ni tofauti kabisa na yule niliyokuwa naongea nae kwenye simu. Kadri siku zinavyozidi kwenda hata suala la kuyaweka mahusiano wazi lilikuwa linapelekwa mbali na upeo wa macho yangu hilo likapita likaja.
wala la mimi kuomba nikatambulishwe kwao hilo nalo lilikuja na mengi.
Kila nilipojaribu kugusia hilo swala la mimi kutambulishwa kwao ilikuwa ndio chanzo cha ugomvi mkubwa sana ulioanza kuibua baadhi ya tabia za Patrick ambazo mwanzoni zilikuwa hazipo kabisa, alikuwa anaweza hata kukaa wiki nzima asijibu sms zangu wala kupokea simu zangu, na hata nilikuwa tukikutana kabisa ni
alikuwa ananikwepa sana. Kuna kipindi nilitamani hadi nikamshirikishe mchungaji juu ya swala hili lakini nikakumbuka tulikuwa nje ya misingi na mafundisho ya kanisa tayari tulikuwa tumeshaanza kuzini. Nikajua moyo labda kesho atabadilika kama sio kesho keshokutwa na siku zinazidi kusonga mbele. Miezi mitatu nikiwa kwenye mahusiano na Patrick
kwa mara ya kwanza nikapata mimba,ikabidi nimueleze Patrick juu ya ile mimba lakini ajabu aliikataa kuwa sio mimba yake nikatafute baba wa mtoto atakayezaliwa na wala yeye hahusiki kwa chochote kile juu ya ile mimba. Hapo mimi nilikuwa ni muumini mzuri sana wa kanisa na muimba kwaya niliyeaminiwa hadi na mchungaji na nilibeba dhamana ya kanisa likijua mimi ni kiongozi muadilifu, ni kama tamani nzima ya kanisa ilikuwa mikononi mwangu mwenyewe.
Kila nikiiwazia ile mimba na imani ya watu juu yangu na itakuwaje baada ya kanisa kugundua kuwa nina mimba likaja wazo,wazo lililoletwa na Patrick kama msaada wake wa mwisho kwangu nami bila kipingamizi chochote huku nikiwa na hofu ya kanisa nikalibeba wazo lile na kuliweka mabegani kwa ajili ya kulifanyia kazi. Ni hofu ya kanisa ndugu msomaji sio hofu ya Mungu.
Niliogopa kanisa na maneno ya watu kuliko hata nilivyomuogopa Mungu wangu.
Lilikuwa ni wazo la kuitoa ile mimba kabla haijawa kubwa na watu kuweza
kuishuhudia,nilianza kutumia vidonge ambavyo nililetewa na Patrick.Ni kama vilikuwa na nguvu sana kuna muda niliumwa lakini nilijikaza kuonekana nipo imara,kuna wakati niliuweka uhai wangu mpakani mwa uzima na mauti lakini hofu ya kuaibiki iliizidi hofu ya kifo.Baada ya
mwezi mmoja hali yangu ikarudi kawaida kama mwanzo.
Mapenzi upofu, huu msemo kwa wakati ule ulikuwa unafanya kazi kwangu kwa mda huo na mimi ndio nilikuwa kipofu mwenyewe. Baada ya magumu yote hayo niliyoyapitia lakini bado Patrick alikuja kuniomba msamaha na nikamuelewa kwa kisingizio kile kile cha shetani alinipitia nikasahau kuwa sio kila nyakati shetani humpitia mwanadamu, zipo nyakati mwanadamu
analazimika kumpigia shetani. Hilo litapita…
*********
Siku zikaenda hatimaye mwaka mmoja ukawa umetimia tangu niwe katika mahusiano na Patrick.Katika mwaka huu wa pili ni Kama Mungu alitaka anionyeshe ya kuwa naweza nikawa mfu na bado natembea, naweza nikamtegemea mwanadamu na bado nisipate nilichokitaka.
Nakumbuka ilikuwa ni usiku wa mkesha wa Christmas ndio nilimuaga Mama naenda kwenye mkesha wa Christmas kanisani lakini ukweli ni kwamba nilikuwa nimeenda kwa Patrick usiku wa siku ile. Mungu ananjia nyingi za kumuumbua mwanadamu lakini hoi haikuwa njia bali adhabu kamili.
Kwa mara ya kwanza nagundua hata Patrick kumbe nae anakunywa pombe,ndio lilikuwa ni jambo lililonishangaza sana lakini bado na mimi nikaionja pombe siku ya usiku ule. Nilionja pombe kwa ushawishi wa Patrick, nilikuwa tayari kukufuru Mungu lakini sio Patrick ila mapenzi…
Sikuonja uchungu wa pombe peke yake bali nilionja hata uchungu wa kufanyiwa kitendo cha kinyama ambacho sijawahi fikiria kama nitakuja kufanyiwa vile na mtu niliyemuamini kupitiliza.
Baada ya kunywa pombe mno usiku ule nilijikuta nafanya mapenzi na wanaume zaidi ya mmoja, Walikuwa wanaume wanne na wote ni rafiki zake na Patrick,nilifanyiwa kitendo cha kinyama ambacho hata kwa kushtaki nilikosa hilo likawa doa la kwanza kwenye maisha yangu ambalo halitakuja kufutika hata kwa jik.
Kitu kimoja ambacho unatakiwa uzingatie ni kwamba ukiwa mwovu unaishi kwenye kivuli cha mtu mwema sana kuna matendo utafanyiwa na utashindwa kwa kwenda kushtaki ili tu kukilinda kivuli chako cha wema. Nilirudi nyumbani nikiwa namachungu na majuto huku nikiamini huenda ni malipo ya kuwadanya nipo kwenye mkesha wa Christmas ilihali nilikuwa kufanya uwovu.
Kwa mara nyingine Patrick akarudi kuniomba msamaha na kuzitupia lawama zote pombe lakini safari hii nilikuwa na moyo mgumu mno na hatimaye nikayavunja mahusiano yangu na
Patrick rasmi.Wiki ya kwanza ikaisha vizuri kabisa ikafungamana na wiki ya pili kabla ya tatu haijabisha hodi ilianza kuonyesha dalili mbaya mapema kabisa Mara uchovu,mara kutapika,mara kichwa kinauma hapo nikahisi jambo ambalo hata kabla sijahisi sikutaka liwe kama nilivyohisi,kuna muda nilipingana na hisia zangu lakini kuna wakati ilibidi niukubali uhalisia.
Sikutaka niziamini hisia zangu nilienda moja kwa moja hadi hospital na kupima ili nijue kama ni sawa na nilivyohisi. Kwa mara ya kwanza nikapata mshtuko ambao nilitakiwa kuupata pale nilipojihisi nipo.
tofauti.Lilikuwa ni tatizo lililomuhitaji Patrick kwa kiasi kikubwa sana kuliko wakati wowote ule.
Nilikuwa nina mimba ambayo hata sikujua baba wa mtoto ni nani kwani hawa watu nilio lala nao sikuwakumbuka hata kwa sura tu sembuse majina yao.
Kipindi natoa mimba ya kwanza nilijiapia kuwa siwezi kutoa mimba nyingine ile ni ya mwisho lakini leo nakuja kujua kuwa siwezi nikaishi kwenye vifungo nilivyovitengeneza mwenyewe.
Kuna wakati inabidi tuishi nje ya ahadi zetu tulizojiwekea kuzifanya hata kama tukiwekewa mdomo wa bunduki kichwani. Baada ya kugundulika nina mimba niliita halimashauri ya kichwa changu ili kujua tunafanyaje. Kabla sijaondoka eneo la hospital nilihakikisha nimechukua namba za daktari wa kiume na kweli nilifanikiwa katika hilo.Sikutaka zipite siku nyingi .hapana usiku ule ule nikaongea na Doctor
kuhusu kuitoa ile mimba mwanzo ilikuwa ngumu lakini alikubali kwa sharti la kushiriki nae
mapenzi kabla hajanihudumia.
Hapo nikawa katika njia panda ya nimtafute nani Patrick kwa ajili ya kumwambia ukweli au nimfuate doctor kwa ajili ya kuitoa mimba yangu ya pili.
Ni Kama nilikuwa kwenye ndoto mbaya na yakutisha iliyojaa wahusika wenye roho mbaya na katili.
Niliona ni kama hata nikimtafuta Patrick haitasaidia chochote hivyo ilikuwa imebaki njia moja tu kuificha hii aibu.Sikutaka ichukue muda mrefu nikiwa na kiumbe yule tumboni hivyo siku mbili mbele nilienda kuonana na doctor Yule kisha tukatekeleza ukatili wa kukitoa kiumbe kile tumboni kisicho na hatia ikawa ni mimba yangu ya pili kuitoa. Nilitoa mimba, sio mimba tu nilitoa na penzi pia.
Hii ilikuwa ni tofauti na ya kwanza kwani hii sikuumwa wala kupata usumbufu wowote ule. Maisha yakaendelea huku kwa wakati huu nikiwa makini na wanaume sikutaka yanikute Kama yaliyonikuta kwa Patrick. Miezi ikasonga huku nikiweka ahadi ya kuwa nikipata mwanaume sitoruhusu tushiriki chochote hadi pale atakaponiowa. Hilo lilikuwa Dhoruba namba moja toka niwe na umri ambao Serikali inaniruhusu kuolewa likapita kisha likafuata lingine.
SEHEMU YA TATU
(Mpaka hapo mimi nilikuwa nimeelekeza umakini wote kumsikiliza yeye ambaye alikuwa ananipa story ya yaliyomtokea hadi akachagua kazi ya uchangudoa.Zilipita dakika tatu kisha akaendelea)
Peter huyu ni mwanaume wa pili kumjua toka nimetimiza miaka kumi na minane achana na Peter yule wa kwanza huyu ni peter mwingine kabisa.Alikuwa mkaka mpole, huyu nilikutana
nae tulivyoenda kanisani kwao kwenye semina ya vijana ndio siku tuliyokutana na tukabadilishana namba kisha tukaanza mawasiliano.
Ni aina ya wakaka waliokuwa wanajali sana,huyu nilianzisha nae mahusiano miezi mitatu baada ya kukutana nae.Hapa sikutaka kuwa na haraka kama nilizozifanya kwa Patrick kwanza nilianza kumchunguza ni mtu wa aina gani kisha nikapima uvumilivu wake kwa kuchelewa kumpa jibu langu.
Taratibu nikaanza kusahau yale niliyopitia wakati wa nyuma na kuanza kufungua moyo wangu kwa Peter.Nilibadili ratiba kila jumapili nilienda kusali kwao ibada za jioni na hapo nikamjua vizuri Peter.
Mapenzi yananguvu sana, kwa muda huo nilikuwa tayari nimesahau maumivu niliyoyapitia nyuma na kujiona sasa Mungu amenipa sehemu.
salama.Kitu ambacho nilikuwa sijakijua bado ni kwamba ile likizo ambayo moyo wangu ulipewa sasa ilikuwa mbioni kuisha.
Miezi mitatu inayounda robo mwaka ikashikamana na mingine mitatu sasa ikaunda miezi sita. Peter alikuwa ni mwanaume wa tofauti na wale niliowapata mwanzo, hakuwa na haraka sana hata lilipokuja suala la mimi kutambulishwa kwao alikuwa muelewa sana. Tulikaa na tukapanga mwezi mmoja mbele ndio safari ya kwenda kutambulishwa kwao iwe kisha yeye kwetu baada ya hapo tufanye sherehe ya uchumba kisha harusi.
Hatua za awali zilifuata na kukamilika zote bila pingamizi lolote, kwa hilo namshukuru Mungu ziliisha salama likaja swala la kufunga harusu tukio lililokuja na majuto mengi yasiyo na mfano.
Nakumbuka wakati ikiwa imesalia wiki moja tu kukamilisha siku ambayo naisubiri kwa hamu ubwa nilipokea ujumbe uliokuwa na kila harufu ya kuyavunja mahusiano yangu kama tu nisipomtafuta aliyetoa ule ujumbe.
Sasa nilikuwa nipo katika hatua za kuyapigania mahusiano yangu kutoka kwa mtu nisiyemjua na wapi kapata habari zangu zinazoweza kuhatarisha mahusiano yangu. Sikuwa na muda wa kupoteza kwani ilikuwa ni kama karata yangu ya mwisho naicheza huku nikiwa na asilimia chache mno za kufanikiwa.
Ule ujumbe niliopokea siku ya kwanza ulikuwa unanitaka mimi nikutane nae niliupuuzia kwa kudhani labda hauna umuhimu wowote lakini ulipokuja kwa mara ya pili ukiwa na sura yake halisi ulinifanya nihisi hii adhabu niliyopewa ni kubwa mno siwezi kuhimili radha yake japo sekunde tu.
Mara ya kwanza nilipokea ujumbe kwa namba ngeni ukinitaka tukutane tuongee suala langu kabla siku ya harusi haijafika nikapuuzia lakini ujumbe wa pili uliotumwa kupitia WhatsApp ndio ulinifanya mimi nimtafute mwenyewe muhusika wa ile namba kabla mambo hayajawa makubwa.
Nilikuwa nimetumiwa picha zangu za utupu nikiwa kitandani na wanaume tofauti tofauti watatu hapo nilikuwa sijajua zile picha wamezipata wapi Nilikuwa nakimbizana na mambo mawili kwa wakati mmoja, Kwanza nakimbizana na muda pili nakimbizana na suala la picha zangu zisivuje.
Hawakukosea walio sema mshika mawili moja humponyoka hata hivyo kwangu hilo moja kilikuwa mbioni kuniponyoka. Kila muda nilikuwa nawaza sana zile picha zangu zimepigwa wapi hadi pale iliponijia kumbukumbu ya iliyopotea kichwani miaka mingi iliyopita.Ilikuwa ni sura ya Patrick imekuja kwa njia nyingine kabisa njia ambayo sikutaka
itokee tena.
Haraka haraka nilifungua mtandao wa WhatsApp kisha nikaitafuta ile namba ambayo ilinitumia picha nikatuma ujumbe wa maandishi wa kujua yeye anataka nini ili zile picha asifute zote kwa ajili ya usalama wangu na maisha yangu ya ndoa.
Saa moja mbele ule ujumbe nilioutuma whatsap ulikuwa tayari umesomwa na jibu limetumwa, hakuwa anataka kingine zaidi ya mimi na yeye tukutane tuongee hilo halikuwa swala gumu kwangu nikakubali na tukapanga eneo la kukutaniana.
Walishasema wahenga jambo usilolijua ni kama usiku wa giza ni mimi kwa wakati huo nilikuwa nipo katika hilo giza, nilikuwa naelekea kuolewa na Peter huku bado kivuli cha Patrick kikiwa kinanitafuta kwa kasi kubwa sana.
Siku ya kuonana na mmiliki wa namba ili ilipofika nilijiandaa ilipotimu saa moja kamili jioni
nikaanza safari iliyonipeka kwenye guest moja iliyopo mtaa wa pili na hapo nilielekezwa hadi chumba ambacho muhusika yupo nilienda moja kwa moja huku swali kichwani likiwa ni nani naenda kukutana nae ni kama fumbo lililonisumbua kwa muda mrefu sasa lilikuwa linaenda kufumbuliwa Nikafika mlangoni nikanyonga kitasa ikiwa ishara ya kuufungua mlango nao ukatii ukafunguka taratibu nikaanza kuingia ndani kwa hofu iliyoubeba mwili wangu huku moyo ukiwa na shauku ya kujua ni nani huyu.
Macho yangu yalibaki kama yameganda, ni kama lilikuwa ni shambulio la ghafla lililorudishwa kwangu wakati mimi nilikuwa nategemea mpira umeisha niliishiwa nguvu kisha miguu nayo
ikanitupa sakafuni nikadondoka….!!!
SEHEMU YA NNE
MIAKA MITATU NYUMA.
Ilianza kama utani kwa mzee Yule kunitaka kimapenzi alikuwa ni mzee wa umri sawa na baba yangu mzazi, japo yeye alikuwa ni mwenye pesa na mwingi wa mali alisifika sana kwa tabia zake za kutembea na mabinti wadogo pale mtaani na hakuna aliye mtaka akakataa.
Kadri muda ulivyozidi kwenda hatmaye na mimi niliingia kwenye anga zake, haikunishangaza sana mzee huyu kunifuata na kunipa ahadi kede kede maana niliijua tabia yake ya kuwalaghai mabinti ambao wapo katika rika langu hivyo nilijitahidi
kumkwepa kadri ya uwezo wangu wote.
Kila njia aliyotumia kuniweka ndani ya mchezo mimi niliiwahi kuigundua kabla yake,hakutaka kushindwa alijiapiza kwa viapo vyote lazima anipate.
Maisha nayo yalizidi kusonga hadi siku moja usiku aliponipa lift kwenye gari yake, nilikuwa
naelekea kanisani kushiriki ibada ya mkesha wa pasaka kwakuwa nilikuwa nimechelewa nae akatokea kwa njia ya kunipa msaada sikuwa na pingamizi lolote nikaingia ndani ya gari safari ya kuelekea kanisani ikaanza hatukwenda umbali mrefu sana ila ilikuwa ni kati kati ya kiwanja, gari ikasimama kisha akaanza kunilazimisha tufanye mapenzi huku akiniahidi kunifungulia biashara kubwa na kubadilisha maisha yangu lakini moyo wangu ulikuwa ngumu sana hadi alipojaribu kunibaka nilipiga kelele kubwa mno iliyomshitua hata yeye mwenyewe, kuna watu walikuwa wanapita karibu na eneo lile kwa kuhisi wanaweza kusikia sauti yangu akaniacha niende huku akiweka ahadi ya kuwa nitajutia kwa yote niliyoyafanya. Jumapili kadhaa mbele ndio Patrick alikuwa mgeni aliyehamia kanisani kwetu kisha nikaingia nae katika mahusiano nae,Sikujua kama ulikuwa ni moja wa mpango wake au mpango wake ulikuja mbele.
Nikiwa pale chini kumbukumbu zote zilipita kichwani na sasa nilianza kumuona muhusika wa mambo yote yaliyoniyokea katika maisha yangu.
Aliponiona nikiwa nimedondoka chini kama mzigo alinifuta na kuniinua kisha akanambia
“karibu”, sikuwa na jinsi nilisimama na kuenda moja kwa moja kitandani na kukaa
“Kwani unataka nini”lilikuwa ni swali la kwanza hata kabla ya salamu kwani nilianza kuiona dalili ya hatari hata kabla ya hatari yenyewe.
“Hadi unafika hapa nadhani unajua kilichokuleta, ni chaguo lako”aliongea na kuiacha sentence yake ikiwa bado hewani iliimalizia
“Unaendelea na msimamo wako tutoe picha au unafanya kilichokuleta”
Aliongea bila hata chembe ya huruma kwamba mimi naweza kuwa hata mwanae wa kumzaa kama sio wa pili basi wa tatu.Sikuwa na
msimamo wowote kwa wakati huo ni kama alikuwa ameshika mpini na mimi nimeshika
makali kwa namna yoyote ile maisha yangu yapo hatarini kama atakua kuvuta tu ule mpini.
Sikuwa na namna siku tatu kabla ya harusi yangu nikavunja uaminifu wangu ambao hata Peter bwana harusi mtarajiwa nilimnyima hio nafasi ya kufanya hivyo.
Niliondoka pale kwa namna moja moyo wangu
ulikuwa na majuto huku namna nyingine nilikuwa nina amani ya kuweza kuifunga ndoa yangu kwa amani kabisa pasi na mashaka yoyote. Sikujua kuwa hayo yote ilikuwa ni kama sijaingia kwenye mchezo kamili nilikuwa naandaliwa labda pengine nije kuwa na uzoefu wa kuhimili
mchezoni kwa muda mrefu.
Masaa yakaenda na siku zikasogea hadi pale siku ya harusi ilipowadia, ilikuwa ni siku iliyoanza na dalili za mvua kwangu ilikuwa ni siku iliyoanza vizuri kabisa hakukuwa na kiashiria chochote kibaya.Tulipomaliza kanisanai hatmaye tukaenda ukumbini kisha fungate yetu tukaenda kuimalizia katika hotel iliyopo nje ya mji wetu.
Siku za fungate zilianza na nilikuwa na furaha sana huku nikiamini nimeishinda mitihani yote sasa naenda kutulia katika ndao yangu bila ya shaka yoyote ile.Kwa upande wangu jahazi ilianza kuingiza maji wiki ya pili baada ya fungate. Kwanza sijawahi shiriki tendo la ndoa kabla na mme wangu tumeenda kushiriki katika fungate yetu lakini mbona kama naanza kuona dalili siyo za kawaida kabisa na hapo awali Kwa Mara ya kwanza nilimkumbuka Mungu wangu kwa kilio kikubwa sana nikimuomba aniondolee hii dhahama inayonikabili maana kama ni mateso basi nishateseka vya kutosha kwa nini haya yawe makubwa hivi. Zile dalili hazikuwa kwangu tu hata kwa mume wangu zilionekana moja kwa moja ni tofauti na
mimi ambaye niliweza kuzihisi mwenyewe tu lakini kwa mume wangu zilionekana bila
kipingamizi chochote.Ulikuwa ni ugonjwa wa zinaa ambao ulikuwa umeanza kuyashambulia maungo ya mwanaume wangu
Swali la kwanza lililokuja kwangu ni kwamba niliupata siku ile guest au nilikuwa nao toka zamani na nitatokaje kwenye huu mtego bila kuhisiwa kuwa nilimsaliti kabla ya harusi yetu,
Kuna muda hata Mungu hutusikiliza sisi waja wake lakini katika maombi yangu niliombea janga moja tu huku nikisahau la pili lililokuja na dhoruba ya kuvunja jahazi ya ndoa yangu.
Baada ya kugundulika na ule ugonjwa wa zinaa ilitulazumu tuende moja kwa moja hadi katika hospital kupata matibabu ya haraka sana na kwa hilo tulifanikiwa tukapewa vidonge vya matibabu huku kwangu vikija na mashart ambayo yaliibua hisia mbaya kichwani kwangu Ilikuwa ni baada ya kupata majibu Mume wangu alitoka nje kuongea na simu mimi nilibaki na doktari kuchukua maelezo ya jinsi ya kutumia vidonge vile, kwa mume wangu alitakiwa atumie dozi ya kawaida tu ila mimi ilibidi nibadilishiwe dozi tofauti na yake kwani niliambiwa ya kuwa vile vingine haruhusiwi kutumia mama mjamzito. Kwa mara ya kwanza nilihisi hakuna usawa duniani hata mbinguni katika hesabu zangu katika mzunguko wa hedhi nilikuwa nimeingia fungate siku salama hii mimba imetoka wapi tena hata kabla sijaongeza neno na mume wangu akawa anaingia….!!!
SEHEMU YA TANO
Bado nilikuwa nipo katika hesabu kali kichwani mwangu, nichukue dawa niondoke tukutane na Peter njiani kabla hajamfikia doctor au nimsubiri hapa hapa. Wazo la kumsubiri niliona ni kama kujichimbia kaburi mwenyewe, nilichukua dawa na kunyanyuka kwa mwendo wa haraka na kukutana na Peter hata kabla hajamfikia Doctor. Kilichonisaidia ni kwamba nilikiwa nimelipia Dawa mapema hivyo hakukuwa na sababu za yeye kwenda kule kama maelezo nilikuwa
nimeshapewa tayari. Safari ilianza kurudi katika Hotel tuliyofikia,
tulimalizia Fungate yetu na sasa ilikuwa ni muda wa kurudi nyumbani. Safari iliyochukia masaa kadhaa tukawa tayari tumefika nyumbani kwa Peter ambapo nilitakiwa kuishi nae kwa ahadi ya kifo kututenganisha. Mwezi mmoja ulitosha kuonyesha dalili zangu za ujauzito ambazo zilianza kujionyesha mapema sana Safari hii niliamua kuishi na hii Mimba hata mtoto atakapozaliwa kwani nilishatoa mimba mbili nyuma hofu yangu nikitoa na hii naweza poteza kabisa kizazi changu hivyo hii ilikuwa iwake jua inyeshe mvua, afe kipa afe beki, nakubaliana na yote nitabaki na hii mimba hadi mwisho wake. Ilikuwa ,,kni taarifa ya kufurahisha baada ya mimi kubeba mimba, kwa pande zote mbili taarifa zilipokelewa kwa furaha sana lakini kwangu Mimi nilikiwa ni kama nimebeba mzigo mkubwa usioweza kuelezeka.
Siku nazo zikazidi kusogea mbele kwa wengine waliona ni kama siku zinachelewa ili waweze kukiona kilicho tumboni wakati kwangu niliona siku zinaenda kasi zaidi ya mshale uliorushwa nyikani.
Miezi mitatu ilitimia, haikuja peke yake bali ilikuja na matukio yaliyoiweka roho yangu mpakani, Lakini richa ya yote hayo niliweza kutoka salama hakika pale niliuona mkono wa Mungu ukinipigania hivi kama mimi ndio last born wake.
Ilikuwa ni tatizo lilolosababisha ndoa yangu kwenda mrama, katika miezi mitatu hio nilipata homa ya ajabu sana ambayo sijawahi jua ilitokea wapi nilipelekwa hospital nililazwa mwezi mzima nikiwa hoi bin taabani, Bado unataka kujua kama niliendelea kubaki na mimba au ilitoka.
Ile homa ilinichukia mwili wangu wote na kila kilichopo mwilini, kama damu niliongezewa, kama maji pia niliongezewa hata ile mimba ilitoka sasa nikabaki mimi kama mimi. Kutoka wa ile Mimba kwangu ilikuwa ni kama nafuu ya kuyaanza maisha mapya yasiyo na matatizo tena lakini sikujua huo ndio ulikuwa mwanzo wangu wa Mimi kuishi maisha ya dhiki ambayo hayategemei faraja.
Hapo ndio ukawa mwanzo wa Mimi kushika mimba na kuporomoka, kila mimba ilifikisha miezi mitatu inatoka hapo ikabidi nianze matibabu haraka sana na kuhudhuria clinic kila nikiwa na mimba lakini haikusaidia kitu. Nakumbuka mimba iliyokaa muda mrefu ilikaa miezi tisa yote, lakini nilifungua kwa operation kinachoniumiza kila nikiangalia huu mshono ulionitesa miaka miwili ni kwamba walimtoa mtoto akiwa hayupo hai tena na huo ndio ukawa mwisho wangu wa mimi kubeba mimba.
Niliamua kuchukua maamuzi ya milele, niliamua kufunga kizazi maana niliambiwa kama hii mimba imetoka na uhai wa huyu mtoto basi ukiendelea kupata mimba zaidi zitatoka na uhai wako.
Yote yakapita maisha yakaanza tena, lakini hakuna maisha magumu kama maisha ambayo unajua mume wako anatoka nje ya ndoa tena hatumii Kinga. Najua utajiuliza nilijuaje hatumii Kinga nitakujibu kwa sababu alikuwa anatafuta mtoto maana kwangu ilikuwa imeshindikana kumpata kabisa.
Pale ndio nililiona joto la jiwe kwanza mawifi kila kukicha wananisimanga na kunitukana, kingine
Peter alikuwa anaweza kukaa hata siku tatu nje akija usimuulize chochote ukimuuliza tu ugomvi unaanzia hapo, mara ya kwanza niliwaambia nilikonda kwa sababu ya kuumwa sasa safari hii nilikonda kwa sababu ya maisha magumu ya ndoa. Hakuna kitu kilikuwa kinaniumiza kama kuwaona walioharibu maisha yangu wao walikuwa wanaishi maisha mazuri na amani kabisa, niliumia mno.
Ikafika wakati nikawa sipati tena huduma ndani na kwakushitaki kulikuwa hamna na ni wakati
huo Peter alikuwa amepata mtoto na mwanamke wake wa nje, kuna siku nilifanikiwa kusikia Peter akiongea na ndugu zake kuwa Mimi nifukuzwe ili wamlete yule mwanamke aliyemzalia mtoto.
Na hapo kwa upande wangu nikaamua kucheza karata, nikawa nimebakiwa na kadi moja tu
nikawaza niitupe au nichange tena….!!!
SEHEMU YA SITA
Kadri muda ulivyozidi kwenda nayo ndoa ikazidi kuwa kifungo kigumu nilichochagua mwenyewe. Sikutaka kuonekana sivumilii mengi, nilivumilia kila aina ya vituko na kejeli ambavyo nilifanyiwa ila sikutaka kuiacha ndoa ipotee mabegani
mwangu ule msema wa mvumilivu hula mbivu ulikuwa ukaa kama nyota kwenye bega la
mwanajeshi mwenye vyeo vingi.
Hakika kadri muda ulivyozidi kwenda niliamua kuungana na wahenga kuuafiki ule msemo wa ndoa ni Ndoano. Nakumbuka siku moja baada ya wiki mbili kupita bila mume wangu kuja kwanza walianza mawifi kuweka kambi kabla sijapokea ugeni ulionikumbusha ya kuwa bado mkononi nipo na karata zangu na sijachukua maamuzi sahihi.
Peter alikuwa amerejea na mwanamke wake aliyemzalia mtoto wake, kwa mara ya
kwanza ndani ya nyumba ile niliiona radha ya kulala chumba cha wageni ingali mimi ni mwenyeji,
ulikuwa ni usiku mrefu na mfupi kwa wakati
mmoja kuna muda niliona masaa hayaendi na kuna muda niliona mshale wa saa unakimbia mno, ule muda nilioamua kulala niingoje kesho ndio niliona mshare wa saa unatembea polepole, nilipoamka na kuzichanga karata zangu niliona Muda unakimbia mno ni kama sasa mshale wa saa ulikuwa unazunguka kama feni mbovu.
Hapakuchi panakucha, walishasemaga wazee wa zamani usiku wa deni hauchelewi kufika hatmaye asubuhi ilinikuta ndani ya nyumba yangu lakini hii asubuhi sikutakiwa kuamka kama mama mwenye nyumba nilitakiwa nijichagulie upande wa kukaa, upande wa kuwa wifi au upande wa kuwa mfanyakazi mle ndani
nikachagua kuishi kama mfanyakazi huku nikisubiri muda wangu huenda Mungu atanibariki katika haya ninayoyapitia. Wiki tu ilitosha kunifanya nione nyumba yangu ni kama uwanja wa vita, siku tatu za kushinda nikilia zilikiwa tayari zimeshanipa majibu ya kwenda kutafuta makazi mapya sehemu nyingine mbali kabisa na ile nyumba, Safari ya kwanza ilikuwa ni kurudi nyumbani kwetu ambapo hapakuwa mbali sana maana tulikuwa tunaishi mji mmoja ilikuwa ni safari iliyojaa visa na visasi moyoni mwangu na hapo niliamua nikiwa hai sitakubali wabaya wangu waishi wakiwa hai niliamua kujichimbia kaburi kwa mikono yangu mwenyewe.
Patrick ndio jina ambalo lilikuwa linakizunguka kichwa changu kwa muda mrefu, Safari hii niliamua nimtafute mwenyewe ili nianzishe mahusiano nae tena.Mahusiano yaliyokuwa na kila dalili ya kunitia hatarini hatari kubwa kuliko zote nilizopitia huko mwanzo.
Ilinichukua wiki kurudiana na Patrick ambaye alikuwa yupo katika hatua za mwisho kabisaa za kufanya harusi yake na mpenzi wake. Niliingia kwenye Yale mahusiano kwa makubaliano ya mimi kubaki kama mchepuko wake tu na
atanitafuta akinihitaji sio mimi nikimuhitaji nilikubaliana na kila shart alilonipa nilikuwa kama kondoo aliyeelekezwa kibra lakini nyuma ya yote hayo nilikuwa nimebeba kisasi kizito sana moyoni mwangu laiti angelijua yaliyokuwa yamefichwa nyuma ya tabasamu langu bandia asingekubali hata kuweka ukaribu na mimi.
Hakuna aijuaye kesho, Siku tatu kabla ya harusi yake Patrick aliniita Lumumba hotel, nami bila kuwaza mara mbili niliona ile ndio ilikuwa nafasi yangu ambayo niliingojea kwa muda mrefu nafasi ya kumaliza yaliyomo moyoni mwangu.
Ilikuwa saa tatu usiku, nilivalia ijabu iliyofunika mpaka macho yangu kisha nilivaa suruali iliyonishika mwili wangu vilivyo niliongoza hadi chumba ambacho alikuwa anataka tukutane nami nikafanya hivyo.
Niliingia na kumkuta akiwa tayari ameagiza chakula na vinywaji akiendele kunywa taratibu nami pia niliungana nae huku tukipiga story za ndoa yangu ambayo nilikuwa nimemdanganya ya kwamba nimerudi nyumbani kwani kuna matatizo yalikuwa yametokea.
Saa nne bado tulikuwa tupo ndani ya kile chumba, kichwani nilikuwa nasubiri kosa moja lifanywe na Patrick japo lilichelewa lakini ikafanyika, Patrick alitoka nje kuongea na simu na kuviacha vinywaji vyake vikiwa wazi kabisa na hapo niliamua kufanya kitendo ambacho hata
ujasiri sijui niliupata wapi kwa wakati huo.
Niliweka sumu kwenye glass yake,sikutaka sumu imuuwe pole pole nilitaka ikiwezekani imuuwe mbele ya macho yangu, kilikuwa ni kidonge ambachu kikiwekwa kwenye kinywaji chochote kinayeyuka kwa haraka sana.
Nilipokiweka kidonge kwenye chupa yake nacho kilitii kilipotea kwa haraka kama kipande cha barafu mchana wa jua kali la saa saba. Ilikuwa sasa ni kumsubiria Patrick aje iwe ni mwanzo wa
kisasi changu chenye mafanikio.Dakika kadhaa mbele Patrick alilejea japo
alikuwa na haraka kidogo aliniaga ya kwamba ameitwa mahali fulani hivyo hataendelea kubaki pale, nami kwa sauti ya upole nilimsihi japo amalizie kile kinywaji tu huku nami nikimalizia chakula changu.
Alinikubalia bila kujua anajiingiza kwenye mtego yeye mwenyewe, aliichukua chupa kabla hajanywa simu ikaita tena hapo akaipokea huku mkono mmoja ameshika simu huu mwingine ameshika kinywaji hapo yakawa ni maombi yangu yatimiye ni kama hata muda ulisimama kupisha jambo lile lenye kuweka roho mkononi lifanyike.
SEHEMU YA SABA
Kuna muda hata mapigo yangu ya moyo waliacha kupiga na kuna muda roho ya huruma iliniambia
nifanye kitu lakini bado hata mimi nilikiwa nipo njia panda.
Ni kama mchezaji anayesubiriwa kupiga penaty ya mwisho ipigwe ndio ilikuwa kwa upande wangu nasubiri jambo langu litimie huku nikiwa katika hali ya huruma. Peter alichukua glass na kupiga funda moja kisha aliongeza na ya pili.Hapo moyo wangu sasa ulianza kujutia kwa yale malipo niliyoyafanya lakini nikiacha itoke kwa maana nilikuwa nimepitia mazito sana ambayo yaliondoa kila chembe chembe ya huruma katika nafsi yangu.
Kwa mwendo wa haraka Peter alitoka nje na kuingia katika gari yake, nilimuona kupitia dirisha akiwa namwendo wa haraka kidogo kisha
kuchukua gari yake na kuondoka kwa kasi sana, sijajua alikuwa anakiwahi kifo chake mwenyewe au alikuwa anawahi nini, lakini alikuwa na haraka sana.
Asubuhi kabisa mji ulikuwa upo kimya sana, ni Kama mitaa ilikuwa inanong’ona ila haitaki kupaza sauti kila sehemu kulikuwa na minong’ono inayohitaji umakini mkubwa kuisikia.
Sasa hatimaye hata ile minong’ono Ikawa sauti, Zilikuwa ni habari za kifo cha Peter aliyekufa kwa ajali ya gari yake mwenyewe. Vyanzo vingi vilikuwa vinadai ulikuwa ni mwendo kasi alikokuwa nao dereva wakati wa kuendesha gari lakini chanzo changu kiliniambia huende alizidiwa nguvu na ile sumu hivyo kushindwa kulihimili gari ipasavyo.
Kuna muda moyoni nilijutia na kuna muda nilihisi nimetua mzigo wa dhambi mkubwa sana, sasa
ikawa ni muda wa mimi kupumzika na heka heka za huku na kule. Baada ya kifo cha Peter sasa nilikuwa nipo salama na moyo wangu ulilejesha amani wenyewe na hapo maisha yalianza kurudi kama kawaida tu, Sikutaka tena kuanzisha mahusiano na watu wa karibu na mji ule hivyo ilinilazimu nihame mji niende kwa shangazi mkoa mwingine.
Miezi mitatu katika mji wa ugenini niliona kama nimefika peponi, kwanza kila kitu kipya hata watu niliokutana nao walikuwa wengine kabisa na anayeifahamu historia yangu alikuwa ni shangazi tu kwa upande wa mjomba sidhani kama alikuwa anajua.
Hapo napo nikaanza kusali, lilikuwa ni kanisa lile lile nililokuwa nasali mwanzo safari hii nilikuwa makini sana na waumini wenzangu kwa sababu yaliyonikuta mwanzo yalinipa funzo kubwa sana.
Mwaka mmoja ukaisha salama. Lakini kwa upande wangu nami nilihitaji kuwa na biashara kidogo ya kufanya na nitaipata wapi na mtaji sina hapo kikawa kitendawili kingine, nilienda
nikaongea na shangazi juu ya hilo wazo la mimi kuwa na biashara lengo langu lilikuwa ni yeye
anikopeshe mtaji kidogo wa kufanyia biashara.
Nilikuwa na mpango wa kuanza kuchukua vitenge na kukopesha kwa watu mbali mbali, shangazi alinambia ngoja kwanza aongee na mjomba ili wajue watanisaidiaje nami nikakaa kusubiri
majibu ya msaada niliouhitaji. Wiki moja baadae haikuwa kawaida ya mjomba kuwahi kurudi nyumbani kabla ya shangazi lakini siku hii yeye ndie alikuwa wa kwanza
kufika,alinikuta nikiwa namalizia kuandaa chakula cha jioni . Aliniita sebuleni na kusema anamaongezi na mimi, baada ya kumaliza kupika nilienda kumsikiliza mjomba kwani ilikiwa ni mara ya kwanza kuniita huku shangazi akiwa hayupo.
Sikuwa na mazoea nae kabisa kwani mazoea yetu yalikuwa ni kwenye salamu basi.
Siku hio mjomba aliongea mengi sana, licha ya kuongea mengi pia alinigusia na swala la mtaji ya
kwamba hatanikopesha Bali atanipa kama na mimi nikiwa tayari kufuata vile yeye anataka.
Shetani akiamua akufuate katika maisha yako hakuna namna unaweza kumkimbia nakwambia, hili jaribu lilikuwa ni tishio sana heri yale niliyoyakimbia huko nyuma lakini hili lilikuja kwa style ya kuvutia na kuogofya kwa wakati mmoja.
Ni kama utajiri uliokuja ukiwa ndani ya jeneza, hapo ni wewe kuuchukua au utaacha kwa sababu upo ndani ya jeneza.
Naaam Mjomba alikuwa anataka tuingie kwenye mahusiano ya kimapenzi aliahidi kunipangia nyumba, kunifungulia duka la nguo kama tu nitakubali kuwa naye pia aliahidi ya kuwa itakuwa siri sana kati yetu na yeye tu.
Kichwani nilijua fika ya kwamba hakuna siri ya watu wawili,kwa wakati huo sikujua kati ya utu na tamaa kipi nikiweke mbele,lilikiwa ni jambo baya katika mwonekano wa kuvutia.
Nilimuomba anipe mwezi mmoja tu utatosha kumpa jibu lipi nifanye na lipi niache lakini kichwa changu kwa wakati huo kilikuwa ni kama kipo njia panda ya kutoa majibu.
Kwa wakati huo sikuwa na rafiki, sio wakati huo hadi sasa sina rafiki, yupi ningemshirikisha hili swala basi ni kamati ya ubongo wangu tu ndio iliyohusika kutoa majibu.
Yalikuwa ni majibu ambayo hata mimi yalinishangaza hata ule mwezi nilioomba nikaona ni mrefu sana, siku ya tatu tu nikachukua simu na kumuandikia mjomba ujumbe, ujumbe uliozua taharuki nyingine kubwa kuliko hizo nilizozipitia nyuma..
SEHEMU YA NANE
Kama wasemavyo wajuzi wa mambo usiku wa deni hauchelewi kufika, nami niliona ule mwezi
niliompa ni kama kifungo ambacho mejifunga mwenyewe sasa niliamua kukikata kwa mikono yangu, bila kulazimishwa na mtu.
Nilimuadikia SMS mjomba ya kuwa nimekubali kuwa namahusiano nae kwa shart moja tu, shart la kutimiza ahadi zake alizoniahidi kama nitaingia nae kwenye mahusiano. Kwa mjomba hilo
halikuwa taabu kwake maana alikuwa ni mtu mwenye uwezo mzuri tu kiuchumi hivyo hata mimi sikuwa na shaka yoyote.
Wanasemaga siri ni ya watu watatu kama wawili watakuwa wamekufa, kwangu hii haikuwa na maana yoyote ile kwani kwa viapo vyote niliahidi kuilinda siri ile kwa gharama yoyote hata kama itahitajika uhai wa mtu. Mahusiano yakaanza rasmi Mimi na mjomba.
Ndani ya mwezi mmoja tu nilikuwa
nimefunguliwa duka la nguo huku Shangazi
akijua ni mkopo niliokopa kwa rafiki yangu huko
nyumbani nilikotoka laiti angeijuia siri iliyopo nyuma ya yote hakika asingeweza kuvumilia.
Mwezi wa pili nilitoka kwa shangazi na kwenda kujitegemea, yote haya sikuweza kutafanya mimi ni mjomba ndio aliyekuja na wazo la mimi
kwenda kujitegemea pia ni yeye aliyenitafutia chumba na kulipa kodi pamoja na kuweka kila kitu.
Kwangu niliona ni kama bahati ya mtende kuota jangwani, wazo la kusema kwamba natoka na mume wa mtu tena mume wa shangazi yangu
likatoka na sasa mjomba. nikamuona kama mume wangu na shangazi ni kama mke
mwenzangu tu.
Kadri siku zinavyozidi kwenda kuna mmea ulianza kuota kwenye moyo wangu na kadri
ninavyoukausha ili usistawi nao unakuwa kwa kasi, ni WIVU wa mapenzi sasa ulianza
kujengeka moyoni mwangu, ni kama mjomba ni mme wangu sasa anachepuka kwa shangazi.
Hapo kumbuka sikuwa na mwanaume mwingine zaidi yake, hivyo muda ambao nilitumia kuwa nae ni mchache sana huenda ikawa hata wiki inaisha tusionane na tukionana hatamaliza hata masaa matatu anaondoka.
Ule upendo ambao mjomba alikuwa anauonyesha kwa mke wake sasa nilitaka na
mimi niupate kama shangazi anavyoupata. Wivu ulikuwa ni mkubwa kuliko upendo wangu kwakwe kila nilichokuwa nakifanya kwa mda huo
kiliongozwa na wivu na sio mapenzi.
Ilibidi nibadili ratiba zangu za kusafiri kwenda kufuata mzigo na sasa zikawa sawa na za
mjomba hapo kidogo nilipata mda wa kuwa nae, ilifiki kipindi tukiendaa kufunga mzigo tunakaa wiki nzima hili hata shangazi lilimtia hofu lakini hakuweza kuelewa ni kipi kinaendelea.
Shangazi yangu aliniamini sana ilifika kipindi alikuwa ananambia nimchunguze mme wake akisafiri anakuwa na nani kwani kipindi cha hivi karibuni amebadilika sana na anahisi anaweza kuwa na mwanamke mwingine, angejua kuwa kikulacho ki nguoni mwako kamwe asingenipa ile ruhusa ya kumchunguza mjomba.
Siku nazo hazikuwa nyuma sana kwani kadri muda ulivyozidi kwenda nami nilizidi kuzama kwa mjomba,ile hofu ya siku moja kushikwa na haikuwa upande wangu tena.
Miezi ikaenda hatmaye tena nikashika mimba,hii haikuwa mara ya kwanza kushika mimba nadhani ni kipindi ambacho kiliamua kufungua kizazi changu baada ya muda mrefu. Hizi habari za
mimi kuwa mjamzito kwangu hazikunishtua Lakini kwa mjomba ilikuwa tofauti sana. Kwake ilikuwa ni kama kupewa habari ya kutisha na kuogofya sana, toka nilivyompa taarifa hizi niliona amepoteza amani kabisa hata ule ukaribu na mimi sasa ukaanza kupungua. Baada ya mda kupita hatmaye mjomba alikuja na sera zile zile za nyuma tuitoe mimba.
Kwangu nilijua hii mimba haiwez kuvuka miezi nane lazma itatoka tu,hivyo sikuwa na wasiwasi hata chembe hata nilivyomueleza mjomba kidogo ikampa amani maisha yakarudi kama awali.
Miezi ilikuwa inasonga na hatmaye miezi tisa ikatimu na bado nikiwa na mimba ile, hapo hata mimi sasa hii hali ilinichanganya itakuwaje mtoto akizaliwa jamii itanionaje, shangazi na ukoo kwa ujumla utanichukuliajee haya maswali
yalinikosesha amani kabisa.
Siku nazo hazigandi, ule usiku niliiuogopa ukafika hatmaye nikashikwa na uchungu hapo sikuwa peke yangu katika hili hata shangazi yangu alikuja kuniuguza kabla sijaenda hospital
kujifungua………
SEHEMU YA TISA
Nilifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume,ni kama Mungu aliamua kudhihirisha ule msemo
walionena wahenga, hakuna Siri ya watu wawili. Ni kweli mtoto alikuwa kachukua kila kitu kutoka kwa mjomba Jambo ilionyesha dhahiri mtoto ni wa mjomba lakini shangazi aliendelea kunihudumia hadi tunatoka hospital .
Wiki ya kwanza iliisha vizuri, lakini wiki ya pili mtoto aliugua ghafla na kupelekea kufarika. Hili likawa ni pigo kubwa sana kwangu hata yule mtoto ambaye nilijua atanipa faraja sasa hayupo tena.
Maneno ya watu yalikuwa mengi sana kuhusu yule mtoto, lakini wakati wote huo shangazi yangu alikuwa kimya japo ukimya wake ulinitesa lakini maneno ya watu yalinitesa zaidi.
Maisha yakaendelea, jambo la ajabu ni kwamba sikukoma kuwa na mahusiano na mjomba nayo mahusiano yetu yaliendelea kama kawaida. Sijui kwa shangazi ilikuwaje maana ilifika hatua kila mtu alijua ya kwamba mimi natoka na mjomba lakini shangazi bado aliendelea kuwa kimya bila kusema lolote.
Kama kuna kitu kilikuwa kinanitesa na ule ukimya wa shangazi na furaha pindi nikiwa nae, sijajua ni kipi kilikuwa kinaendelea ndani ya nafsi yake, hakika kimya kingi kinamshindi mkuu.
Ilikuwa ni kawaida yangu kila nikitoka kazini lazima nipitie bar ninywe kidogo bia kisha nianze kurudi kwangu,hii tabia ikawa kama utaratibu wangu niliojiwekea kila siku.
Siku moja nikiwa njiana narudi usiku saa tatu ilikuja gari mbele yangu, alikuwa amepanda
mkaka mmoja mtanashati hivi akaniomba anipe lift nami kwakuwa nilikokuwa naenda ni mbali niliona kama baraka imeshuka mbele yangu. Kawaida yangu huwa natumia boda boda kurudi nyumbani, siku hii boda boda wangu alinambia ya kuwa anaumwa hivyo nitafute sehemu nyingine ambaye anaweza kunifikisha nyumbani.
Basi nikiwa ndani ya lile gari dereva wake alikuwa busy sana kuendesha hivyo sikupata hata muda wa kuongea nae. Katika kumbu kumbu zangu sikumbuki ni nini kilitokea nikiwa nipo ndani ya gari ila ninachokumbuka ni kama kuna mtu alitokea
nyuma yangu na kuniziba na kitambaa usoni na hapo nikapoteza fahamu. Nilikuja kushtuka nikiwa nipo hospital huku mikononi zikiwa zimefungwa drip za maji yakiendelea kushuka taratibu kuingia mwilini.
Katika kipindi chote hicho nikiwa hospital hata shangazi yangu hakuja kuniona nilikuwa nahudumiwa na mtu mmoja tu, hata mimi nilikuwa simfahamu ila alikuwa ni mdada mmoja aliyekuwa ananiletea chakula kila jioni na
mchana.
Mwezi mmoja ukatima na hali yangu sasa ilikuwa imeanza kutengamaa, nilichukuliwa na yule
mwanadada na kupelekwa kwake anakoishi yeye, kila nilipohitaji kwenda kwangu alinigomea sana alihitaji niishi kwake mule ndani tena kwa Siri sana hata watu wasijue kama nipo mule ndani.
Basi maisha yakaendelea kama kawaida, nilikuwa napewa kila kitu ilihali sijui vinatoka wapi hadi siku nilipoambiwa Yule dada yeye kaajiliwa tu kunihudumia hadi hali yangu utakapo kaa vizuri ndipo nitaonana na mwenyeji wangu. Nikaongeza mwezi mmoja wa kuisubiri hali yangu
itengamae basi hata siku ilipofika ya mimi kuonana na mwenyeji wangu.
Kama ningejua kuwa ile shauku ya kuonana na mwenyeji wangu ni sawa na kukifuata kifo basi ningeachana mara moja na ile hamu ya kujua ni nini kipo nyuma ya haya mambo yote yanayotokea …
SEHEMU YA KUMI
Hakika hawakukosea waliosema usilolijua ni kama usiku wa Giza, hatmaye siku ya kuonana na Mwenyeji wangu iliwadia. Ilikuwa ni siku niliyoisubiri kwa shauku kubwa sana,sikujua ni siku iliyoenda kunipa majuto ya milele na ilikuwa ni siku ambayo mambo yote yaliyopo nyuma ya maisha yangu nilienda kuyajua na kuyaelewa.
Ilikuwa saa kumi na mbili jioni, nilipopewa taarifa za mwenyeji wangu kuwepo maeneo Yale, nilitoka chumbani kwangu kwa shauku kubwa sana hadi sebuleni ambako kweli nilimuona mgeni wangu
Ilikuwa sura ngeni kabisa machoni pangu ambaye sijawahi muona kabla, huu niliona ni kama jaribu lingine sasa ambalo sijajua litatokea wapi.
Swali lilikuwa kichwani mda huo ni kwamba nitahudumiwaje na mtu nisiyemjua na anataka nini kwangu tena. Basi baada ya kufika sebleni nilimsalimu na kusubiri nipewe maelekezo nijue nini cha kufanya. “Naitwa Kiza, naaam najua utakuwa umeshtuka kuniona hapa na najua hii sura ni ngeni kwako mimi nimetumwa kama muwakilishi tu na Rasco”yalikuwa ni maneno ya utangulizi lakini yenye kila dalili ya kuwa huenda nilikuwa mikono salama sasa.
Rasco ni mjomba wangu ambaye kwa mda huo niliambiwa alikuwa amesafiri ameenda kuchukua mzigo . Rasco alinieleza mengi sana lakini ya muhimu kuliko yote ambayo Rasco alinambia ni hii story iliyopo nyuma yangu.
Anasimulia Kiza..,
“Mpaka leo upo umri huo umfahamu baba yako” aliniuliza Kiza
Nilitikisa kichwa kutoka kulia kwenda kushoto kumaanisha hapana simfahamu kwani alikufa mimi nikiwa mdogo sana sikubahatika kumuona.
“Nyuma ya maisha yako kuna siri nzito sana imejificha, Yule unayejua ni baba yako sio baba yako japo mama yako alifanya siri sana watu wasijue cha ajabu hata baba yako hajui kama wewe ni mwanae. Mama yako kipindi mume wake anaumwa sana alitoka kimapenzi na mzee Reck, unamjua”
“Hapana simjui”nilijibu
“Yule mzee tajiri pale kijijini kwenu ulipotokea, alikuwa mfupi hivi anakitambi anapenda sana kutembea na visichana vidogo hivi”
Moyo wangu ulitamani kama upasuke lakini ni kwa wakati mmoja nilikuwa nisiyaamini mawazo yangu, jibu lililokuwa linakuja sikutaka kulikubali ilihali ndio jibu lililokuja kwa usahihi kabisaaaa.
“Inamaana yule mzee mpuuzi ndio mzee
wangu, inamaana….”kilio cha kwikwi kilianza kunitoka huku nikijaribu kuvuta kumbu kumbu zilizoniumiza Mara mbili, kumbukumbu chafu ambazo zimegoma kufutika hadi leo
“Ndio yule ndio mzee wako, huyu mzee masuti
aliyekufa wakati wewe mtoto hakuwa mzee wako yule”Kiza aliongea
Niliishiwa nguvu kila nikikumbuka tayari nishafanya mapenzi na baba Yangu mzazi,
hakika nilimlaani baba yangu mzazi pamoja na vizazi vyake vyote.
“Ndio mbaya zaidi ni kwamba alikufa wiki mbili nyuma, hatunaye tena duniani na amekufa akiwa bado hajui kama wewe ni mwanae. Hilo ni la kwanza ambalo wewe ulitakiwa ulijue .
La pili ni kwamba uko kwenu saivi wanajua wewe ulishakufa toka siku ile umetekwa, Maana ile ilikuwa ni Njia ya shangazi yako kulipa kisasi alichokifanya alituma watu wakuchukue wakuuwe kisha wakuzike yaani hakutaka hata kuiona maiti yako, mwanamke anaroho mbaya sana yule.
Uzuri ni kuwa wale watu walikuwa wanafahamiana na Rasco hivyo walikujeruhi tu na kumuita Rasco aje akuchukue. Ndiyo huyo Rasco aliyekupeleka hospital na kukutafutia mtu wa kukuhudumia, huko kwenu taarifa zilizopo kuwa wewe ulishakufa na kila mtu anajua hilo kasoro mimi na Rasco na wale waliotumwa kukuuwa.
Cha mwisho lile duka lako, Rasco alihamisha vitu na kuviuza alichukua hela akaenda mkoa mwingine kukupangia nyumba na kukutafutia biashara ya kufanya hivyo utaenda kuishi huko, hii leo mimi nakutoa na kukupeleka huko ila yeye atakuja baada ya mwezi mmoja kukupa maelezo mengine”alimaliza Kiza kuongea Ilikuwa ni simulizi iliyokuwa imejaa machungu na visasi hapo nilikuwa sina hamu ya kuendelea kuishi haya maisha yaliyojaa DHORUBA isiyokuwa na mwisho.
Baada ya maelezo yale tulitoka pale na kuelekea mkoa huu ambao nipo sasa, hapo nilipewa nyumba iliyokuwa na kila kitu mule ndani isipokuwa amani ya moyo wangu tu.
Hakuwa amenipangia nyumba kama alivyosema awali bali alikuwa amenunua nyumba ambayo ndio hio naishi mpaka sasa kwa hilo namshukuru Mjomba sana.
Kati ya watu ambao nilikuwa nawasiliana nao ni Kiza pekee yake hakuna mwingine.
Mwezi mmoja ulipita na wa pili pia, Baada ya mwezi wa pili nikitafutwa na mjomba na kunambia anakuja mwezi huu kuja kunikabithi biashara ya kufanya kwani ameenda kuchukua mzigo wangu
Basi siku iliyokuja na jambo la kushangaza ilikuwa jumatano asubuhi nilipokea simu kwa Kiza juu ya kifo cha mjomba wangu aliyekufa kwa ajali ya gari wakati anarudi kutoka kuchukua mzigo.
Ilikuwa ni habari iliyobadilisha maisha yangu hadi Leo hii unaniona nimeamua kufanya kazi hii.
Ni wiki sasa inaisha toka Mjomba wangu afariki, Kiza bado naendelea kuwasiliana nae lakini naona hana msaada na mimi tena japo aliahidi kunisaidia ile hela ya kutumia nimebakiwa na akiba chache sana sina na namna ya kufanya Zaidi ya hii kwani kama maisha ya ukahaba nilishayaishi hata kabla sijawa kahaba. Najua bado unajuiliza wewe umekuwaje mteja wa kwanza, ni kweli jana nikiwa mtandaoni ndio niliona hii app ambayo inatumiaka kufanya hii biashara na mimi nilifuata hatua zote za kujiunga na hata mpaka saivi nimehitajika sehemu zaidi ya tano lakini kwa bahiti nzuri nikawa nimechagua wewe uwe mteja wangu wa kwanza.
Alimaliza kusimulia Agnes.
“dah pole sana Agnes kwa hayo yaliyokukuta,umepitia magumu mengi sana lakini hujakata tamaa bado unaishi”
“Asant Pocha”aliongea agnes huku akifuta Machozi
Kwa wakati ule sikuwa na haja tena na mwili wake bali nilikuwa nimeweka utu mbele kwanza kuliko kitu chochote, nilimpa hela na hapo niliahidi kurejea kwake kwa wakati mwingine.
Nilimuomba aacha biashara anayoifanya, alikubali akaacha na alikaa kwake nami
kwangu hadi siku nilipopata mtaji kidogo kwa kushirikiana na kiza tulimfungulia
biashara ya nguo tena.
Baada ya miaka mitatu aliolewa, tatizo lake la mimba liliisha baada ya kwenda kufanyiwa matibabu ikiwa ni pamoja na kusafisha kizazi
Sasa hivi ni mama wa watoto watatu kati ya hao kuna mmoja anaitwa RASCO.
MUNGU AKUBARIKI.

Comments
Post a Comment