Posts

Showing posts from May, 2024

JINSI NILIVYOJIFUNZA KUACHA KUDHARAU MAMBO MADOGO

Image
Siku Moja ya Tarehe 25/5/2024) Nikiwa Safarini,Barabara ya Kwenda Dodoma Eneo la Makuti, Kulikua na Matengenezo ya Barabara,Kiasi cha Magari Kutakiwa Kuchepukia Barabara ya Vumbi. Dereva Alichepusha Gari Kuacha Barabara ya Lami(Barabara Kuu)Kuingia kwenye Vumbi(Barabara ya Muda),  Nikiwa katika Hali ya Usingizi,Nikaskia "Dereva Angalia! Dereva Angalia!" Ilikua ni Sauti ya Mama Mmoja aliekua Karibu na Dereva,  Nilishtuka sana,nikafungua macho Kuona nini Kinaendelea, Kumbe yule mmama alikua anamkumbusha dereva no 2( Konda),Kua Afunge Dirisha la Mlango wa Kuingilia,  Dirisha Lile lilikua Linapitisha Vumbi Ndani ya Gari, Nilishangaa sana,Nikatabasamu Kidogo "Mh😊! Nikasema Moyoni,"Vumbi ndio ya Kumshtua Hivyo Huyu Mama!?"  Badae Kidogo Nikatulia ili Kutafakari ni Kitu gani naweza Kujifunza Kupitia Kauli ile,Hatujawahi Kuskia Watu Wamekufa Kwasababu Vumbi ilijaa ndani ya Gari, Lakini Tumewahi Kuskia Vumbi Ilikua Kubwa na Kusababisha Dereva Asione Vizuri(...