WALINICHOMA KISU MARA NNE
Naitwa Moza, ni msukuma wa Bariadi. Sawa , mwaka 2022 nilimaliza chuo DUCE nakumbuka wiki moja kabla sijamaliza mtihani wangu wa mwisho wa UE, nilipigiwa simu na shangazi yangu aishiye Iringa mjini kwamba nimalizapo mitihani niende iringa nikamtembelee. Nikaona ni vyema sana maana mara ya mwisho yeye kuja Bariadi ilikuwa kipindi niko sekondari. Iliniongezea ulazima wa kwenda maana shangazi pia alikuwa amefiwa na watoto wake watatu tena vifo vya kutatanisha. Hivyo mimi kwenda ilikuwa namna pia ya kumtia moyo. Miaka yote nilipokuwa nakua, kwenye familia yetu kulikuwa na migogoro kati ya ndugu upande wa baba na upande wa mama . Nilikuwa sielewi nini haswa kilitokea huko nyuma . Nilijaribu kumuuliza mama shida ni nini lakini mama alinisihi kupuuza tu maisha yaendelee.
wiki moja baadae nilikuwa nimeshamaliza mambo yote ya chuo. Nilipanda bus mpaka Iringa. Baada ya kufika Iringa shangazi alikuwa ameshanijulisha kuwa atamwagiza dereva ambaye ni rafiki yake anifuate anipeleke hadi nyumbani kwake.
sawa muda si muda yule dereva alinipigia kunijulisha kuwa amekaribia stend na kweli si muda alifika. Alinipokea alikuwa amevalia jaketi jeusi lilivofunika mpaka shingoni, pia alikuwa na miwani myeusi pia alitia kofia kubwa ya mviringo kwaiyo sikuweza kumuona usoni vizuri. Aliondoa gari tayari kuelekea kwa shangazi.
Cha ajabu badala ya gari kuelekea mjini ambako ndiko najua shangazi ndo anaishi, gari likashika njia ya vumbi kuelekea mbali na mji . Nikawaza huenda shangazi alihama. Safari ikaendelea kama nusu saa nzima, gari liliendeshwa kwa kasi na dereva alipandisha vioo na ku-lock milango . Moyo ulianza kukosa amani na kuingiwa na hofu kubwa sana . "Mh Hatujafika tu?" niliuliza bila kujibiwa chochote. Nilichukua simu yangu nimtumie SMS shangazi, ujumbe haukwenda. Nilijaribu kumpigia, hakupatikana . Duh, akili ilichoka. ilikuwa inaingia mida ya saa moja usiku na sehemu tuliyokuwa tumefika ilkuwa kama vichaka vichaka nje ikionesha kuwa makazi ya watu hayakuwa karibu. Gari lilikuwa linakimbia kwa kasi ya upepo na dereva alikuwa hazungumzi chochote.
nilichukua tena simu niampigia shangazi, simu yake ikawa haipatikani, na hapo nilipanik nikaanza kulia na kupiga kelele na kumwambia yule mwanaume anishushe. Nilipiga kelele yeye hakujali aliendelea kukanyaga mafuta.
baada ya muda niliona watu mbele ,wanaume watatu na mwanamke mmoja. Nilimfananisha na shangazi na kweli baada ya kushushwa na wale wanaume nilithibitisha kuwa kweli alikuwa ni yeye. walivuruta kwa nguvu na kunifunga kamba. "mama yenu sianajifanya mjanja? tutaona" Shangazi alisema. Nikapigwa na butwaa nikashindwa kuongea maana mdomo na mwili wote vilikuwa vinatetemeka sana . Wanaume wawili huku wameshika visu walianza kuniburuza pembeni ya njia kuelekea kichakani. Nikaanza kumwita Yesu aniokoe. Nilikuwa nakemea kwa nguvu zote mwili ukiwa haujiwezi huku nikilia ."mshughulikieni huyo" Shangazi aliamuru.
waliniacha na mmojawao akainua kisu, alishusha kisu moja kikapenya kwenye misuli ya mkono wangu (bicep), akashusha kingine kwenye mbavu zangu, na kisu cha mwisho hatari kiliingia kifuani kama sentimita chache tu pembeni ya moyo. Katika hali ya kuweweseka nilihisi hatua zao wakikimbilia gari lilipokuwa na kisha nikasikia sauti ya gari ikiondoka kwa kasi kubwa. Niliendelea kumwita Yesu kimoyomoyo maana kinywa changu kilikuwa hakifanyi kazi tena.
Wakati huo, ni kama sikuwa nahisi maumivu yoyote—isipokuwa tu msisimko mkali wa hofu na mshtuko (adrenaline). Nilisikia damu ikibubujika na nguo zangu zilikuwa zimelowa sana, nikaangalia chini na kuona ikimwagika mikononi mwangu mpaka kutiririka chini.
Niliona sasa maisha yangu yamefika mwisho. Katika hali hiyo niliskia gari kwa mbali likija uelekeo ule ni kama halikuwa gari moja bali na pikipiki kadhaa. Miungurumo ya vyombo hivyo vilikaribia mpaka mahali pale wale watu nisowajua wakatawanjika vichakani wakiwa na tochi zao. Mmoja alikuja uelekeo wangu na kuniona baada ya kumulika. "huyu hapa?" alipaza sauti kuwajulisha wenzake. wakakusanyika na kunizunguka pale nilipokuwa nikigalagala chini kwenye majani.
Mmoja wa wale watu nisiowajua aliliuliza, “Jina lako nani?”—“Minza,” nilijibu .
“Bado anajitambua,” mtu mmoja alisema. Tuondoke naye wakanisogelea kunibeba kuelekea kwenye gari lao huku nikihisi kupoteza fahamu. Sikumbuki kilichofuatia baada ya pale.
@@@@@@
Nilizinduka na kujikuta nikiwa hospitalini. Nilipokuwa nimejilaza pale, tabibu na wauguzi kadhaa walikuja na kunihamisha pale. Nilikimbizwa ndani ya gari la wagonjwa, na nikaamini kuwa maisha yangu tayari yalikuwa mashakani. “huyu dada ana majeraha manne ya kisu—moja lipo karibu sana na moyo jambo ambalo ni hatari sana. inabidi ahudumiwe kwa hali ya dharula sana” daktari mmoja alionya. Nikiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), daktari aliniuliza, “Unaniskia?”—“Ndiyo, lakini nina maumivu makali,” nililia, sasa nikiwa ninayaskilizia maumivu yale yaliyokuwa yameambatana na mateso makali.
“Utakuwa salama, lakini unapaswa kuwa imara.”Nikiwa na hofu kubwa, niliuliza, “Daktari, nitanusurika kweli?”
Alijibu, “Kiukweli, ni hamsini kwa hamsini (50/50). Unapaswa kuwa imara.”
Jambo hilo lilinitesa sana. Nililia na kuomba: “Yesu, tafadhali nakuomba uwe nami. Nisamehe. Nifanye niwe mzima. Amina.” Nilikuwa nimepoteza lita 1.8 za damu na nilikuwa natetemeka sana kama degedege. Kifaa cha kupasha joto kiliunganishwa kwenye kitanda changu daktari alipokuwa akinishona.
Alichunguza lile jeraha la kifuani na kuthibitisha kuwa kisu kiliukosa moyo wangu kwa sentimita moja tu. “Una Mungu sana,” alisema. “Lakini hiki nitakachofanya sasa kitakuwa chenye maumivu makali mno.” Moyo wangu ulijawa na afueni—nilijua nitakuwa hai. (Nilikuwa namwamini Yesu kabla ya hapo, lakini wakati huu ulibadilisha kila kitu.)
Mrija ulitakiwa kuingizwa kupitia kwenye mbavu zangu ili kunyonya damu iliyokuwa kwenye pafu langu lililotobolewa. Hayo yalikuwa maumivu makali zaidi kuwahi kuyasikia maishani mwangu.
Mara baada ya mrija ule kuingia, niliweza tu kunong'ona, “Asante, Daktari. Asante Yesu kwa kuokoa maisha yangu.” Lakini jibu lake liliniacha sina la kusema: “Mimi sikuokoa maisha yako. Yesu ndiye aliyeokoa maisha yako. Natumai utajifunza kutokana na hili—ulikuwa na bahati sana.”
Nililia. Huo ndio ulikuwa wakati niliong'amua kuwa alikuwa Mungu aliyenivusha katika yote hayo.
Walipokuwa wakijiandaa kunihamishia wodini, wahudumu waligundua jeraha lingine—chini ya kwapa langu, ambapo kisu kilikuwa kimepenya moja kwa moja kwenye misuli ya mkono (bicep). Daktari alirudi, akalishona, na hatimaye nikahamishiwa wodini ambapo nilikaa kwa wiki moja.
Siku tatu za kwanza zilikuwa mateso makali. Nilipata shida kupumua, kusogea, au hata kwenda chooni. Lakini nilipata marafiki wodini, na kila siku niliwauliza madaktari kama naweza kwenda nyumbani . Jibu lilikuwa lile lile kila wakati: “Hadi damu yote itoke kwenye mapafu .”
Siku ya tatu, nilipigwa picha ya kwanza ya X-ray. Ilionyesha mabadiliko mazuri, na madaktari walinitia moyo nianze kutembea. Ilikuwa na maumivu na ya kuogopesha, lakini nilijaribu.
Ikiwemo siku ya saba, madaktari walinipa habari njema kwamba hakukuwa na damu tena kwenye mapafu. Nilijawa na furaha kubwa .
Hivi ndivyo Mungu alivyookoa maisha yangu. Na kama alifanya hivyo kwangu, anaweza kufanya hivyo kwako pia.

Comments
Post a Comment