RAFIKI YANGU ASIYEONEKANA KWA MACHO


 “Ndoto! ndoto! siku fulani nilipanga kuamka saa tisa alfajiri kuwa na mda na rafiki yangu asiyeonekana. ilipofika saa tisa juu ya alama nilishtuka. uchovu niliokuwa nao ulinifanya niendelee kulala. ndani ya dakika 37 za kulala huko niliota ndoto ifuatayo….” 

YESU ASIFIWE.,
llikuwa ni usiku mmoja mtulivu majira ya tisa alfajiri nikiwa narejea nyumbani gafla niliona majitu mawili yenye nguvu yamevalia mavazi ya jeshi. bila kujua kosa nililotenda amri ilitolewa nikalala chini kifudifudi na kuchapwa viboko viwili. nikiwa pale chini nimelala pasi kujua hatima yangu niliyaona yale majitu kama yakijadili kufanya ubaya flani. yakiwa yamezubaa nilipata fursa ya kuyaponyoka na kutimua kuvumbi kuendeleza safari yangu kuelekea nyumbani. nikiwa njiani nilipita njia iliyokuwa na maziko na kumkuta mrimbwende mmoja amefichama kando ya mti. 

alivyoniona alianza nishutumu mimi kuwa sababu ya mambo yake yanayokwenda mkama. nilivyomtaka athibitishe amejuaje kuwa mimi ndiye chanzo, alinijibu kuwa amejuzwa na mtaalamu kuwa yeyote atakayepita eneo hilo mda huo ndiye. alianza kukata tawi la mti kutaka kuniadhibu huku amegubikwa na jazba kubwa. 

angali katika jitihada zake za kukwanyua tawi hilo la mti nilipata upenyo wa kutimua kivumbi tena kuendelea na safari yangu. nikiwa katika mbio nilikigeuza kichwa changu kutazama nini kinaendelea, macho yangu yakumuona yule mrimbwende akiwa na mabinti wengine wawili wakinifukuza kwa hasira. niliendelea kukata mbuga kuelekea nyumbani maana nilijua ndiko salama yangu iliko. nikianza kuyaona mandhari ya nyumbani kwa mbali, nyuma yangu wale warimbwende walikuwa wamenikaribia sana. gafla akatokea mwanamume mmoja akawakamata wale mabinti wote kwa wakati mmoja. masikioni mwangu kwa mbali nikawa nawasikia wakimsihi awaachie ili waendelee kunifukuza. mtazamo wa sura yake kama alitaka kuwaachia. nikapaza sauti yangu na kumsihi mwanamume yule nikisema usiwaachie mpaka nitakapokuwa nimeingia mlango wa geti la nyumbani maana nimekaribia sana. nikiwa na mashaka kama atafanya kama nilivyomsihi niligeuka na kumwona kawakamatilia bado. niliendeleza mbio zile kuelekea nyumbani. nilipoanza kuingia maeneo ya makazi majira ya saa kumi alfajiri niliisikia sauti ikitoka redioni. ilikuwa sauti ya mtu akiomba. sauti iliyosikika ilikuwa ya mtu akiomba kwa bidii. miongoni mwa maombi aliyokuwa akiomba ni ulinzi wa Mungu kwa watu wanaopita katika hatari mbalimbali. 

niliendelea kukimbia mpaka nikaingia mlango wa geti la nyumbani salama kabisa. mwili wangu ulikuwa umechoka nikihema kwa nguvu sana. ilikuwa furaha nilipogundua kuwa mlango wa kuingia ndani ya nyumba pia ulikuwa wazi sikuhitaji kuita mtu kunifungulia. niliingia ndani nikiwa salama kabisa. nilianza tafakari jinsi nilivyookoka na mikono ya watesi wale gafla maneno ya kitabu cha Luka 22 yakaanza kunijia kichwani mwangu. mstari wa 40 aliwaambia wanafunzi wake ombeni kwamba msiingie majaribuni. ijapokuwa yeye alikuwa ni Mungu(mtawala) lakini mstari wa 41 unaonyesha mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba. mstari wa 43 waonyesha msaada toka mbinguni ulishuka na kumwezesha kusonga mbele salama katika kusudi la Mungu. 45 na 46 yaonyesha jinsi Yesu alivyopatwa na huzuni kuwakuta wanafunzi wamelala hawaombi. akawasihi tena ombeni msije mkaingia majaribuni. kumbe tukiomba msaada wapatikana na tunavuka salama. USILALE, TUOMBE. 

 #################### 

JE, UNA USHUHUDA AMBAO UNGEPENDA TUUCHAPISHE?? 
 Fanya hivyo ili maelfu wajue mambo ambayo MUNGU alikutendea na kupitia ushuhuda wako  maelfu ya wasomaji  watayashuhudia matendo ya  Mungu uliyenaye. 
Endapo unao Ushuhuda tafadhali BOFYA HAPA

 

Comments

  1. Ninakumbuka Sana jinsi Mungu alivyonitumia wakat ule mpaka sasa

    ReplyDelete
  2. Amina Ushuhuda mzuri Sana unanijenga Kwa kweli, Ubarikiwe sana

    ReplyDelete

Post a Comment