JINSI JENGO LA BWENI LILIVYOPOROMOKA NIKIWA NDANI YA DARI.

"Nilikaa katika dari nikichaji simu yangu. Nilisikia miungurumo kwa mbali, nikidhania huenda bi gari linapita barabarani huko nje. Lakin baada ya sekunde kadhaa, haikuwa miungurumo ya kawaida. Punde si punde, miungurumo ilizidi kuwa mikubwa.."

Bwana Yesu asifiwe sana., 
Naitwa FELIX NTIRUBAZA (Kigoma, Tanzania) ilikuwa ni septemba 2016. Siku moja siku ya jumamosi mchana, mimi na wanafunzi wenzangu wachache, tulikuwa na kipindi cha vitendo maabara (Ilikuwa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, Bukoba mjini). Baada ya kujifunza mida ya saa kumi alasiri, nilishuka mpaka bwenini ili nikapumzike. Bwenini pale, kulikuwa na wenzangu wachache walokuwa wakifanya maongezi tu ya kawaida. Nilifika kitandani kwangu (nilikuwa nalala kitanda cha chini) na kulala. Baada ya kujilaza tu, wazo liliniingia kusema kwamba niende mjini. Lakin nililipinga wazo hilo kwakuwa sikuwa na ratiba yoyote ya kwenda mjini wala sikuwa na jambo lolote la kwenda kufanya mjini. Nadhiri iliendelea kunisihi niamke niondoke niende mjini lakin mwili uligoma sababu ya uchovu, nikaendelea kulala. Baadae, wazo lilibadilika na kuniambia nipande juu ya dari (kwa kuwa tulikuwa tukichaji simu huko ili waalimu wasitubaini pindi wanapofanya ukaguzi) .

Niliamka na kuchukua simu yangu na chaja, kisha nikapanda juu ya dari kupitia tundu tulilokuwa tumetoboa katika pembe ya jengo. Jengo lilikuwa kubwa na refu kwenda juu. Pia lilijengwa kwa mawe. Baada ya kufika huko ndani, nilikaa katika ubao wa kenji na kuchomeka simu katika kebo. Cha ajabu, sikuweza kuiacha simu na kushuka chini, badala yake, niliwasha simu na kuanza kuvinjari mitandaoni. Baada ya kama dakika 10 hivi, Nilianza kusikia miungurumo kwa mbali, nikidhania huenda bi gari linapita barabarani huko nje. Lakin baada ya sekunde kadhaa, haikuwa miungurumo ya kawaida. Punde si punde, miungurumo ilizidi kuwa mikubwa. Ghafla ,ule ubao wa kenji niliokuwa nimekalia, ulianza kutetema na mabati yalianza kupiga kelele kana kwamba gharika ya mawe ilikuwa inamwagwa juu ya paa.Moyo uliruka na kupaniki. 

Sikuwa naelewa kilichokuwa kinaendelea. mitetemo iliendelea kuwa mikubwa na jengo likaanza kuporomoka. Ninachokumbuka tu, ni kuwa ,nilikuwa naanguka chini afu nimezungukwa na mawe, vumbi, mbao, misumari na kila kitu wakati naporomoka kutoka katika jengo hilo refu. Baada ya sekunde chache ,nilijikuta nimesimama mbali nikiangalia nyuma jinsi wanafunzi wenzangu wakilia na kukimbia huku na huko. 

Sikuelewa nilirushwaje mpaka ile sehemu niliyokuwa. Jengo lilianguka. Nilirejea kuongalia wenzangu wale niliowaacha ndani wakifanya maongezi walivyojeruhiwa vibaya. Wengine walipondwa na mwenzangu aliyekuwa analala kitanda changu cha pembeni alivunjika mgongo. Kitanda changu nilichokuwa nimelalia kabla sijapanda darini, kilifunikwa na kifusi cha mawe na kupindwa japokuwa kilikuwa ni kitanda cha chuma. Lakini mimi mpaka mwisho, hakuna jiwe lililonigusa. sikuwa najeraha wala mchubuko katika ngozi. Namtukuza Mungu sana. Mungu akubariki sana.

 


#################### 

JE, UNA USHUHUDA AMBAO UNGEPENDA TUUCHAPISHE?? 
 Fanya hivyo ili maelfu wajue mambo ambayo MUNGU alikutendea na kupitia ushuhuda wako  maelfu ya wasomaji  watayashuhudia matendo ya  Mungu uliyenaye. 
Endapo unao Ushuhuda tafadhali BOFYA HAPA

 


 




 

Comments

  1. Hakika Ni Mungu Anayetenda mambo makuu mno,Jina lake litukuzwe Kwa kukuponya na Ajali๐Ÿ™๐Ÿ™

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SAFARI YANGU YA WOKOVU

NILIVYOTOKA KUWA MUIMBA KWAYA HADI KUJIUZA NA KUKUTANA NA YESU TENA

USHUHUDA WA MAMA MCHUNGAJI