JINSI JENGO LA BWENI LILIVYOPOROMOKA NIKIWA NDANI YA DARI.
"Nilikaa
katika dari nikichaji simu yangu. Nilisikia miungurumo kwa mbali,
nikidhania huenda bi gari linapita barabarani huko nje. Lakin baada ya
sekunde kadhaa, haikuwa miungurumo ya kawaida. Punde si punde,
miungurumo ilizidi kuwa mikubwa.."
Bwana Yesu asifiwe sana.,
Naitwa FELIX NTIRUBAZA
(Kigoma, Tanzania)
ilikuwa ni septemba 2016. Siku moja siku ya jumamosi mchana, mimi na
wanafunzi wenzangu wachache, tulikuwa na kipindi cha vitendo maabara
(Ilikuwa shule ya sekondari ya wavulana ya Ihungo, Bukoba mjini). Baada
ya kujifunza mida ya saa kumi alasiri, nilishuka mpaka bwenini ili
nikapumzike. Bwenini pale, kulikuwa na wenzangu wachache walokuwa
wakifanya maongezi tu ya kawaida. Nilifika kitandani kwangu (nilikuwa
nalala kitanda cha chini) na kulala. Baada ya kujilaza tu, wazo
liliniingia kusema kwamba niende mjini. Lakin nililipinga wazo hilo
kwakuwa sikuwa na ratiba yoyote ya kwenda mjini wala sikuwa na jambo
lolote la kwenda kufanya mjini.
Nadhiri iliendelea kunisihi niamke niondoke niende mjini lakin mwili
uligoma sababu ya uchovu, nikaendelea kulala. Baadae, wazo lilibadilika
na kuniambia nipande juu ya dari (kwa kuwa tulikuwa tukichaji simu huko
ili waalimu wasitubaini pindi wanapofanya ukaguzi) .
Niliamka
na kuchukua simu yangu na chaja, kisha nikapanda juu ya dari kupitia
tundu tulilokuwa tumetoboa katika pembe ya jengo. Jengo lilikuwa kubwa
na refu kwenda juu. Pia lilijengwa kwa mawe.
Baada ya kufika huko ndani, nilikaa katika ubao wa kenji na kuchomeka
simu katika kebo. Cha ajabu, sikuweza kuiacha simu na kushuka chini,
badala yake, niliwasha simu na kuanza kuvinjari mitandaoni. Baada ya
kama dakika 10 hivi, Nilianza kusikia miungurumo kwa mbali, nikidhania
huenda bi gari linapita barabarani huko nje. Lakin baada ya sekunde
kadhaa, haikuwa miungurumo ya kawaida. Punde si punde, miungurumo
ilizidi kuwa mikubwa. Ghafla ,ule ubao wa kenji niliokuwa nimekalia,
ulianza kutetema na mabati yalianza kupiga kelele kana kwamba gharika ya
mawe ilikuwa inamwagwa juu ya paa.Moyo uliruka na kupaniki.
Sikuwa
naelewa kilichokuwa kinaendelea.
mitetemo iliendelea kuwa mikubwa na jengo likaanza kuporomoka.
Ninachokumbuka tu, ni kuwa ,nilikuwa naanguka chini afu nimezungukwa na
mawe, vumbi, mbao, misumari na kila kitu wakati naporomoka kutoka katika
jengo hilo refu. Baada ya sekunde chache ,nilijikuta nimesimama mbali
nikiangalia nyuma jinsi wanafunzi wenzangu wakilia na kukimbia huku na
huko.
Sikuelewa nilirushwaje mpaka ile sehemu
niliyokuwa. Jengo lilianguka. Nilirejea kuongalia wenzangu wale
niliowaacha ndani wakifanya maongezi walivyojeruhiwa vibaya. Wengine
walipondwa na mwenzangu aliyekuwa analala kitanda changu cha pembeni
alivunjika mgongo. Kitanda changu nilichokuwa nimelalia kabla sijapanda
darini, kilifunikwa na kifusi cha mawe na kupindwa japokuwa kilikuwa ni
kitanda cha chuma.
Lakini mimi mpaka mwisho, hakuna jiwe lililonigusa. sikuwa najeraha wala mchubuko katika ngozi.
Namtukuza Mungu sana.
Mungu akubariki sana.
####################
JE, UNA USHUHUDA AMBAO UNGEPENDA TUUCHAPISHE??
Fanya hivyo ili maelfu wajue mambo ambayo MUNGU alikutendea na kupitia ushuhuda wako maelfu ya wasomaji watayashuhudia matendo ya Mungu uliyenaye.
Endapo unao Ushuhuda tafadhali BOFYA HAPA
Mungu mwema
ReplyDeleteHello
DeleteBlessed
ReplyDeleteHakika Ni Mungu Anayetenda mambo makuu mno,Jina lake litukuzwe Kwa kukuponya na Ajali๐๐
ReplyDeleteAsante sana
Delete