JINSI NILIVYOTAHADHARISHWA KABLA YA AJALI
"Rafiki
yangu ambae ni mtumishi wa Mungu, alinionya sana juu ya kudharau ndoto.
Alinisihi tuchukue hatua ya kuomba. Basi, tulichukua wakati tukafunga
maombi.."
YESU APEWE SIFA.,
Mimi ninafanya kazi ya UWAKALA wa mitandao ya simu yaani M-PESA, TIGOPESA, Airtel Money na HALOPESA. Siku moja nikiwa nimelala nikaota ndoto moja ambayo haikunifadhaisha sana na nikaichukulia kirahisi bila tija yoyote.
“Tazama, nilikuwa
katika kibanda changu nikiendelea na kazi yangu ya uwakala kama kawaida.
Kibanda changu kilikuwa mtaani kando ya barabara. Nikiwa ndani ya
kibanda, ilitokea gari likiwa kwenye mwendokasi wa ajabu kana kwamba
limekatwa breki. Lilianguka na kuanza kubiringika kuja uelekeo wa
kibanda changu hali nimo ndani yake. Kabla gari lile halijanifikia,
nilishtuka kutoka usingizini.”
Niliwaza lakini
nikachukulia ni ndoto tu, na asubuhi nikaenda kuendelea na kazi kama
kawaida.
Siku moja wakati napiga storin a Rafiki yangu ambae ni mtumishi wa
Mungu, alinionya sana juu ya kudharau ndoto. Alinisihi tuchukue hatua ya
kuomba. Basi, tulichukua wakati tukafunga maombi kumwomba Mungu ili
kwamba endapo kuna jambo baya limepangwa na adui, lipate kubatilika.
Siku moja, nikiwa kibandani kwangu kama kawaida, nilitoka kidogo nje ya
kibanda kwa dharura ndogo na kwenda katika duka moja eneo la Jirani.
Wakati nimetoka, lilitokea gari mahali kusikojulikana kwa kasi ya ajabu
kana kwamba breki zake zimefeli.
Gari lilianguka na kuanza kubiringika mpaka katika vibanda vyetu.
Nilipata kuokoka kwa kuwa sikuwemo kibandani. Endapo ningekuwemo ningedhurika na hata kupoteza Maisha.
Namshukuru Mungu sana kwa Kuniokoa na janga hilo.
####################
JE, UNA USHUHUDA AMBAO UNGEPENDA TUUCHAPISHE??
Fanya hivyo ili maelfu wajue mambo ambayo MUNGU alikutendea na kupitia ushuhuda wako maelfu ya wasomaji watayashuhudia matendo ya Mungu uliyenaye.
Endapo unao Ushuhuda tafadhali BOFYA HAPA
Mungu mwema
ReplyDeleteIt is a heart -touching message
ReplyDeleteTusipuze ndoto Zina maana kubwa maishani kwetu,najifunza zaidi.
ReplyDelete