TATIZO LINALOWAKUMBA VIJANA WENGI BAADA YA KUOKOKA


 Kuna tatizo sugu ambalo linalowasumbua watu wengi , hususani vijana pindi wanapookoka, Na pengine linakusumbua hata na wewe. Vijana kadha wa kadha waliookoka, wamekuwa wakinipigia simu, wengine wakinitumia meseji wakisema mtumishi, tangu nilipookoka, nimejitahidi kweli kuacha uasherati na kutazama picha chafu (za ngono) mitandaoni, Lakini naona kama ninamkosea Mungu kwasababu, zile taswira za yale niliyokuwa ninayafanya au ninayatazama, zinanijia mara kwa mara akilini mwangu, wakati mwingine hata wakati nikiwa naomba, au najifunza Neno. 

 Hivyo naona kama bado sijakamilika, Mungu hajanisamehe na kuniosha dhambi zangu, najisikia vibaya sana, imenipelekea kukosa nguvu ya kumtumikia Mungu.. Nifanye nini? Kama na wewe umekuwa na tatizo kama hili nataka nikuambie, wewe sio wa kwanza, Biblia inasema mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru.(Yohana 8:32) Jambo ambalo wengi hatufahamu ni kuwa, Utakaso wa Mungu umegawanyika katika sehemu mbili. Upo utakaso ambao utaupokea moja kwa moja siku ile unapookoka Upo utakaso ambao Unachukua muda kutimilika. 

Tukianzana na huo wa kwanza, zipo hali ndani yako, ambazo Mungu anaziondoa, mara moja pindi tu unapookoka, kwamfano kiu ya kutenda yale maovu uliyokuwa unayatenda huko nyuma, kama vile wizi, matusi, uvaaji mbaya, pombe n.k. Lakini upo utakaso ambapo itakupasa upitishwe mahali Fulani kwanza kwa muda, ndipo uwe safi kabisa. 

Na ndio maana utaona katika agano la kale kuna unajisi ambapo ulikuwa ukishatakasika, ilikupasa usubirie mpaka ifike jioni ndio uwe safi, mwingine siku tatu, mwingine wiki mbili, inategemeana na unajisi wenyewe. Utajiuliza ni kwanini usiwe na saa hiyo hiyo?

#################### 
JE, UNA USHUHUDA AMBAO UNGEPENDA TUUCHAPISHE?? 
 Fanya hivyo ili maelfu wajue mambo ambayo MUNGU alikutendea na kupitia ushuhuda wako  maelfu ya wasomaji  watayashuhudia matendo ya  Mungu uliyenaye. 
Endapo unao Ushuhuda tafadhali BOFYA HAPA

 

Comments