JINSI NILIVYOJIFUNZA KUACHA KUDHARAU MAMBO MADOGO
Siku Moja ya Tarehe 25/5/2024) Nikiwa Safarini,Barabara ya Kwenda Dodoma Eneo la Makuti, Kulikua na Matengenezo ya Barabara,Kiasi cha Magari Kutakiwa Kuchepukia Barabara ya Vumbi.
Dereva Alichepusha Gari Kuacha Barabara ya Lami(Barabara Kuu)Kuingia kwenye Vumbi(Barabara ya Muda),
Nikiwa katika Hali ya Usingizi,Nikaskia "Dereva Angalia! Dereva Angalia!"
Ilikua ni Sauti ya Mama Mmoja aliekua Karibu na Dereva,
Nilishtuka sana,nikafungua macho Kuona nini Kinaendelea,
Kumbe yule mmama alikua anamkumbusha dereva no 2( Konda),Kua Afunge Dirisha la Mlango wa Kuingilia,
Dirisha Lile lilikua Linapitisha Vumbi Ndani ya Gari, Nilishangaa sana,Nikatabasamu Kidogo "Mh😊!
Nikasema Moyoni,"Vumbi ndio ya Kumshtua Hivyo Huyu Mama!?"
Badae Kidogo Nikatulia ili Kutafakari ni Kitu gani naweza Kujifunza Kupitia Kauli ile,Hatujawahi Kuskia Watu Wamekufa Kwasababu Vumbi ilijaa ndani ya Gari,
Lakini Tumewahi Kuskia Vumbi Ilikua Kubwa na Kusababisha Dereva Asione Vizuri(Nje ya Gari) na Ajali Kutokea na Watu Kufa,Kuna Mambo Kwenye Maisha yako yanaweza Yasiwe na Madhara ya moja kwa Moja Lakini Yakipitiliza Huleta Madhara,Ndio Maana Kuna Wakati Mungu anatufundisha *KIASI*
Kama Kitu Kinachoweza Kuzaa Madhara ikiwa Kitapitilizwa,Mfano,Usipokua na Kiasi Unaweza Kua Mlevi,Mlafi Nakadhalika.
Naamini Umejifunza Kupitia Shuhuda yangu Hii Fupi.
-Nathanael Shinyanga-
JE, UNA USHUHUDA AMBAO UNGEPENDA TUUCHAPISHE??
Fanya hivyo ili maelfu wajue mambo ambayo MUNGU alikutendea na kupitia ushuhuda wako maelfu ya wasomaji watayashuhudia matendo ya Mungu uliyenaye.
Endapo unao Ushuhuda tafadhali BOFYA HAPA
.
Comments
Post a Comment